Katika jitihada za kukabiliana na kuhimili athari za mabadiliko ya Tabianchi Waziri wa Nchi Ofisi
ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba amesema kuwa Serikali
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itaendelea kutafuta fedha kwa wafadhili na wadau wa
maendeleo ili kupambana na changamoto hii inayoikabili dunia kwasasa.
Waziri January Makamba ameyasema hayo mara baada ya kufanya ziara ya kukagua ujenzi wa
ukuta wa kuhimili wingi wa maji na upandaji wa mikoko katika eneo la Kilimani na Kisakasaka
Unguja.
Athari za mabadiliko ya tabianchi ni dhahiri kwa sasa, sisi kama serikali tunachukua hatua za
dhati ikiwa ni pamoja na kutafuta fedha sehemu mbalimbali duniani ili kuendelea kutekeza
miradi mingi zaidi kama hii ya kupanda mikoko na kujenga kuta zitakazosaidia kupunguza kasi
ya maji kufika kwenye makazi ya watu, Makamba alisisitiza.
Waziri Makamba ameainisha kuwa lengo la Serikali ni kulinda na kuokoa uchumi wa wananchi
wa kuweka miundombinu wezeshi kwa ustawi wa maendeleo endelevu. "ingawa masuala ya
mazingira si jambo la muungano lakini hatuna budi kusaidiana na kushirikiana" alisema Waziri
Makamba.
Nae msimamizi wa mradi huo Mhandisi Khamis Nassoro kutoka Kampuni ya Dezo Civili
Contractors amesema kuwa changamoto kubwa ni uelewa mdogo wa wananchi juu ya hifadhi
ya mazingira na kuwata wananchi wote kufahamu kuwa suala la kutunza na kuhifadhi mazingira
sijukumu la serikali bali ni wajibu wa kila mmoja wetu.
Mradi huo unatekelezwa na Ofisi ya Makamu wa Rais kwa Ufadhili wa Shirika la Umoja wa
Mataifa linaloshughulikia mazingira unatarajiwa kukamilika ndani ya miezi minne na utagharimu
dola za kimarekani 74,166.02
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akikagua
eneo lililopandwa miti aina ya mikoko katika eneo la Kisakasaka Unguja. Azma ya Serikalini kuhakikisha
maendeleo endelelevu kwa wananchi wake ikiwa ni pamoja na kukabiliana na athari za mabadiliko ya
tabianchi. Kulia ni Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mazingira Bw. Sheha Mjaja.
Pichani ni miti aina ya mikoko iliyopandwa katika eneo la Kilimani - Unguja ili kukabiliana na athari za
mabadiliko ya tabianchi. Fedha za kupanda mikoko hiyo ziko chini ya mradi wa Kuhimili mabadiliko ya
tabianchi unasimamiwa na Ofisi ya Makamu wa Rais.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...