Naibu Mkurugenzi Idara ya Habari Maelezo Zanzibar Dr. Juma Mohammed Salum akiwakaribisha wahariri wa vyombo vya habari katika warsha ya siku mbili ya utafutaji Mafuta na Gesi Asilia inayofanyika Hoteli ya Golden Tulip Malindi Mjini Zanzibar.
 Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Maji Nishati na Mazingira Mhe. Ali Khalil Mirza akifufungua warsha ya wahariri wa vyombo vya habari inayohusu utafutaji wa mafuta na gesi asilia katika Hoteli ya Golden Tulip Malindi Mjini Zanzibar (kulia) Prof. Martin Mhando na kushoto Naibu Mkurugenzi Muendeshaji Mamlaka ya Udhibiti wa Utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi asilia Zanzibar Ali Said Bakar.


 Mshauri wa usalama na afya  kwenye mafuta na gesi asilia  Respicious Kundama akiwasilisha mada ya mahusiano ya jamii juu ya athari za mazingira wakati shughuli hizo zikiendelea.
  Mtaalamu wa utafutaji mafuta na gesi asilia kutoka kampuni ya Rakgas ya Rasil Khema Shari Hassan akielezea namna ya shughuli za utafutaji wa mafuta na gesiasilia utakavyofanyika kwa kutumia meli maalumu itakayowasili ijumaa ijayo.
Mwandishi wa habari wa gazeti la Habari Leo  Khatibu Suleiman akiuliza suala katika warsha hiyo inayofanyika Hoteli ya Golden Tulip Malindi Mjini Zanzibar. Picha na Makame Mshenga.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...