Bodi ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma imeagizwa kufanya utafiti wa kina utakaowezesha kuwa na uwiano sawa wa malipo ya mishahara na masilahi ya watumishi wote serikalini.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapteni (Mstaafu), Mhe. George H. Mkuchika (Mb) amesema hayo leo wakati wa ziara ya kikazi katika Ofisi za Bodi ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma jijini Dar es Salaam.

Mhe. Mkuchika amesema kuna baadhi ya taasisi/Idara za Serikali zinalipa watumishi wake mishahara mikubwa tofauti na taasisi nyingine jambo ambalo limekuwa likisababisha watumishi kutotulia sehemu moja na kutafuta masilahi bora zaidi sehemu nyingine.

“Hii haiwezekani, mmesoma darasa moja, fani moja na mko cheo kimoja, lakini mnalipwa mishahara tofauti wakati serikali ni moja, ni lazima mlifanyie utafiti wa kina suala hili. Masilahi ya watumishi wa umma lazima yawe sawa” Waziri
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt.(Mstaafu) Mhe. George H. Mkuchika (Mb) akipata maelezo kuhusu mifumo ya TEHAMA inavyofanya kazi wakati wa mikutano ya kieletroniki (Video Conference) katika ofisi za TaGLA wakati wa ziara ya kikazi aliyoifanya mapema leo jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt.(Mstaafu) Mhe. George H. Mkuchika (Mb) akipokea taarifa (nakala ngumu na laini) zenye shughuli zinazofanywa na Wakala ya Mafunzo kwa Njia ya Mtandao (TaGLA) kutoka kwa Mtendaji Mkuu wa Wakala hiyo, Bw. Charles Senkondo baada ya kumaliza ziara ya kikazi katika wakala hiyo mapema leo jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma, Bw. Donald Ndagula akitoa neno la shukurani kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt.(Mstaafu) Mhe. George H. Mkuchika (Mb) mara baada ya Waziri kumaliza kuzungumza na watumishi wa bodi.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt.(Mstaafu) Mhe. George H. Mkuchika (Mb) akipokea nyaraka mbalimbali zinazohusu utunzaji wa kumbukumbu kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa, Bw. Charles Magaya katika ofisi za Idara hiyo, jijini Dar es Salaam leo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...