Na Sixmund Begashe
Wapiga picha nchini wameshauriwa kutembelea onesho la picha zinazo elezea historia ya maisha ya watanzania Miaka 50 iliyopita ili kujifunza umuhimu wa uhifadhi wa kumbukumbu muhimu za kihistoria ili vizazi vilivyopo na vijavyo viweze kujifunza kwa kuwa Tanzania ya leo sivyo itakavyo kuwa miaka 50 ijayo.
Ushauri huo umetolewa na Balozi wa Denmark Mh Einar H. Jensen kwenye ufunguzi wa onesho maalum la picha zilizo sheheni uridhi wa kihitoria ya maisha ya watanzania miaka 50 iyopita lijulikanalo kama KARIBU TANZANIA lililopo Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam, ambali limeandaliwa na Makumbusho ya Taifa kwa kushirikiana na mpiga picha hizo Bw Jesper Kirknaes
“Picha hizi sasa zimerudi nyumbani Tanzania, baada ya kuwa kwenye nchi za Denmark na Sweden ampapo zilioneshwa huko, niimani yangu kuwa zitakuwa ni mchango mkubwa na muhimu sana kwa Makumbusho ya Taifa, zitatoa nafasi kwa watu kujifunza historia ya maisha ya watanzania na pia zitakuwa ni ushawishi kwa wapigapicha wa hapa Tanzania kuona umuhimu wa kutunza kumbukumbu kwa kupitia picha”. Aliongeza Balozi Jensen

Balozi Jensen alimalizia kwa kuipongeza Makumbusho ya Taifa kwa kazi nzuri ya uhifadhi Uriridhi wa Utamaduni wa Mtanzania, kutumia vyema miundo mbinu na hata kushirikisha wadau katika shughuli za kiutafiti na uwekaji wa maonesho kama ilivyo fanya kwenye onesho la KARIBU TANZANIA.
Akizungumzia onesho hiyo mpigaji wa picha hizo Bw Jesper Kirknaes ameeleza kuwa onesho la KARIBU TANZANIA linaelezea maisha ya watanzania miaka zaidi ya 50 iliyopita, namna walivyo kuwa wakifanya kazi pamoja, walivyo kuwa wakivaa, wakila, na hata kufanya mambo mengine yakimaendeleo kwa ajili ya familia yake na nchi kwa ujumla.

Licha ya kuushukuru Ubalozi wa Denmark nchini kwa kulifadhili onesho hilo, Mkurugenzi wa Makumbusho ya Taifa Prof Audax Mabula ametoa wito kwa watanzania hasa vijana kutembelea Makumbusho kwa lengo la kujionea onesho hilo ili waweze kujifunza historia ya maisha ya watanzania, namna walivyo kuwa wabunifu katika kuanzaisha viwanda.

“Serikali ya awamu ya tano nchini chini ya Rais wetu John Pombe Magufuli, inatupeleka katika uchumi wa kati kwa kuifanya Tanzania iwe ni nchi ya viwanda ifikapo 2020, hivyo si vyema watanzania hasa vijana waka kaa tu bila kujishughulisha kama walivyo jishughulisha watanzania huko nyuma na kuweza kuwa na viwanda vidogo vidogo na hata vikubwa, niimani yangu kuwa onesho hili litarudisha hari kwa vijana ili wawe sehemu ya maendeleo hapa nchini”. Alimaliza Prof Mabula.
Balozi wa Denmark nchini Mh Einar H. Jensen akikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa onesho la KARIBU TANZANIA. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Prof Audax Mabula na kushoto ni mpigapicha mkongwe Bw Jesper Kirknaes.
Balozi wa Denmark Mh Einar H. Jensen akipata maelezo ya picha za kihistoria kutoka kwa mpiga picha hizo Bw Jesper Kirknaes kwenye onesho la KATIBU TANZANIA lililopo Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Jesper Kirknaes ameandika sana kuhusu utamaduni na sanaa ya wa-Makonde. Ninacho kitabu chake kimojawapo. Hao wenzetu wanatuhimiza kuthamini historia na utamaduni wetu, lakini sijui kama tutazingatia. Utamaduni wa kusoma ni kitendawili Tanzania, kuanzia kwa wananchi hadi kwa hao tunaowaita viongozi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...