Msanii wa muziki wa kizazi kipya Benard Paul 'Ben Pol'  (wa pili kushoto) akiwa tayari amewasili katika Jiji la Paris nchini Ufaransa kwa ajili ya kuhudhuria hafla maalumu ikiweo uzinduzi wa Filamu ya NDOTO na kutambulishwa kuwa balozi wa taasisi ya Maüa association.

 Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

MSANII wa muziki wa kizazi kipya Benard Paul 'Ben Pol' ameenda nchinI Ufaransa kwa ajili ya kuhudhuria hafla maalum ya MAÜA Association pamoja na uzinduzi wa Filamu ya NDOTO utakaofanyika Tarehe Novemba 18, 2017 mjini Paris nchini humo.

Ben Pol alisema kuwa tayari amewasili nchini humo kwa ajili ya hafla hiyo iliyoandiliwa na watanzania wanaoishi nchini Ufaransa na  hafla hiyo itaambatana na utambulisho rasmi wa Msanii huyo kama balozi mpya wa MAÜA association.

"Mimi tayari nimeshafika huku na nina matarajio makubwa katika tamasha hili ambalo ni mara ya kwanza kwangu kushiriki katika nchi hii,"alisema.

Alisema kuwa hafla hiyo inatarajiwa kuhudhuriwa na Wana-diaspora, viongozi na wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi.

Maüa association ni taasisi iliyoundwa na Watanzania waishio ughaibuni (Ufaransa). MAÜA association ilianzishwa na kusajiliwa kwa sheria za mashirika ya kujitolea nchini Ufaransa kwa minajili ya kutoa usaidizi wa kiafya kwa watoto na vijana ili kuwasaidia kutimiza ndoto zao. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...