30/12/1935
22/11/2004
22/11/2004
SABINUS PETER KWEKA
Baba yetu
mpendwa, leo umetimiza mwaka wa 13 tangu ulipotwaliwa gafla na Bwana Picha yako
uliyoipiga siku ya mwisho inatukumbusha uwepo wako tulipokuwa sote hapa
duniani, na hasa upendo wako na wingi wa busara.
Ni vigumu
kukubali kwamba haupo nasi lakini hatuna budi kuamini kwamba uko nasi kiroho
kwa vile tunaye Mungu ambaye anaendelea
kututia nguvu kila iitwapo leo. Busara zako zinazidi kutuimarisha kila siku na
tunaendelea kuzingatia maneno yako uliyokuwa ukihimiza juu ya kuwa na umoja
katika familia na upendo kwa watu wote huku tukiendelea kumtumainia Mungu wetu
ambaye amekuita kwake.
Unakumbukwa sana na sisi wanao tuliobaki, JANE,FESTO,EUGENIA,ELIZABETH,CECILIA NA THADEI, Dadako SR. DEVOTHA KWEKA CDNK, WA –
Narumu wote, ndugu, jamaa na marafiki kokote pale walipo.
Misa ya kumbukumbu imefanyika leo – Parokia
ya Mkolani – Mwanza.
Tumaini letu linajengwa na neno lisemalo
“Umevipiga vita vilivyo vizuri, Mwendo umeumaliza na imani umeilinda (2 Tim-4-7)”
Tunaomba
Eee Bwana Uendelee kuipumzisha
roho yake mahali pema peponi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...