Aliyekuwa mbunge wa Songea Mjini (CCM), Leonidas Gama anatarajiwa kuzikwa Jumatatu katika makaburi ya familia yaliyopo Kijiji cha Likuyufusi mkoani Ruvuma.
Gama aliyefariki dunia usiku wa kuamkia leo Ijumaa Novemba 24,2017 atazikwa Jumatatu Novemba 27,2017 katika makaburi hayo yaliyopo umbali wa kilomita 25 kutoka Songea mjini.
Bw. Issa Fussi ambaye ni msemaji wa familia na mdogo wa Gama amesema amefariki usiku wa kuamkia leo akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Misheni ya Peramiho. Amesema Gama alikuwa akisumbuliwa na shinikizo la damu na alipelekwa hospitalini hapo Jumatano Novemba 22,2017 usiku na kulazwa hospitalini hapo.
Fussi amesema msiba huo ni pigo kwa familia kwa kuwa Gama alikuwa nguzo akitegemewa katika masuala mbalimbali ya maendeleo na kifamilia.
Amesema mwili wa marehemu Gama umehifadhiwa katika Hospitali ya Peramiho na utaratibu wa mazishi unaendelea.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...