Mkuu wa Wilaya ya Mbogwe Mh Martha Mkupasi amezindua Ujenzi wa Zahanati ya Shenda ambayo inatarajiwa kujengwa kwa nguvu za wananchi kwa kushirikiana na serikali katika uzinduzi huo mkuu Wilaya ameshirikiana na wananchi kukamilisha zoezi la kumwaga Zege na kuendesha harambee ya kupata vifaa vya ujenzi.

Akiongea wakati wa uzinduzi huo Mkuu wa Wilaya amewataka wananchi wote kutoa ushirikiano wa nguvu kazi kwenye ujenzi wa zahanati hiyo kwani zahanati hiyo itahudumia wananchi wote wa Shenda bila ubaguzi. Mkuu wa wilaya amewasisitiza wananchi wote kuungana bila kuangalia itikadi za chama wala dini .

Pamoja na uzindinduzi huo Mkuu wa Wilaya amemwagiza Mtendaji wa Kata ya masumbwe kugawa zamu za kufanya kazi kwenye zahanati hiyo kwa vitongoji vyote vya Shenda kwani Serikali itagharamia gharama za Fundi tu kazi nyingine zote zitafanywa na wananchi wa kijiji husika ili kupunguza gharama na kwenda na kasi ya mkuu wa mkoa wa Geita inayotaka kila kijiji kumiliki Zahanati yake.

Kwa sasa wananchi wa shenda wanapata matibabu kwenye kituo cha afya Masumbwe ambacho kipo umbali wa zaidi ya kilometa mbili kitu ambacho kimekuwa kikileta changamoto kwa wakazi wa shenda zaidi wakinamama wajawazito na watoto.

Vilevile Kaimu Muhandisi wa Ujenzi bi Filomena Bango amesema Zahanati hiyo inajengwa kwa nguvu za Wananchi ambao mpaka sasa wameshafyatua matofali 300 wameshaleta mawe ya kutosha na wanaendelea kushirikia na fundi . Bi Filomena amesema wananchi watakapoishia serikali itachukua jukumu la kumalizia wananchi walipoishia. 
  Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Mbogwe akimwaga maji kwenye nondo zilizoandaliwa kwa ajili ya msingi wa Zahanati
 Mkuu wa Wilaya y a Mbogwe Mh Martha Mkupasi akikagua matofali yaliyofyatuliwa na wananchi kwa ajili ya ujenzi wa Zahanati ya Shenda
 Mkuu wa Wilaya ya Mbogwe Mh Martha Mkupasi akihutubia wananchi wa kijiji cha Shenda wakati wa uzinduzi wa waujenzi wa Zahanati ya Shenda
Wananchi wa Kijiji cha Shenda wakishirikiana na kuchanganya Zege litakalotumika kujenga zahanati ya Shenda

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...