Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
WAZEE nchini wameiomba Serikali kuhakikisha elimu ya haki za binadamu na misingi ya utawala bora inatolewa kwa wananchi wote ili kujenga jamii inayoheshimu haki za binadamu hasa wazee. Pia kuendelea kuboresha huduma za afya kwa wazee ikiwamo upatikanaji wa dawa za magonjwa yanayosumbua wazee.

Hayo yameelezwa Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Shirika la Wazee Mkoa wa Morogoro, Samson Msemembo wakati akitoa  ujumbe maalum ulitolewa na Wazee nchini kuelekea maadhimisho ya Siku ya haki za binadamu duniani ambayo hufanyika kila ifikapo Desemba 10 ya kila mwaka.

Amesema Wazee ni vema wakapaza sauti zao kuiomba  Serikali kufanya mambo mbalimbali yakiwamo ya kushiriki kikamilifu mchakato wa kuanzisha mabara ya wazee nchini ili kujenga mfumo imara  wa uwakilishi.

Msemembo amesema  Serikali kutoa pensheni jamii kwa wazee wote nchini na kuharakisha upitishaji na utekelezaji  wa mkakati wa kitaifa wa kuzuia unyanyasaji na mauaji ya wazee kwa imani za kishirikina .

"Tunatoa shukrani kwa Serikali kuendelea kushirikiana na wadau wa masuala ya wazee katika kutafuta ufumbuzi wa matatizo ya wazee,"walisema wazee hao kwenye ujumbe wao kwa Serikali.

Aidha amesema  kuelekea kilele cha maadhimisho hayo ni muhimu kutathimini hali halisi ya utekelezaji wa haki za binadamu kwa makundi mbalimbali wakiwamo wazee.

Amesema Kauli mbiu ya siku hiyo kwa mwaka huu inatoa wito kwetu kusimamia usawa , haki na utu wa binadamu.

Nae  Katibu wa Mtandao wa Mashirika ya Wazee , Wilson Kaluwisa  ameiomba serikali  kuzingatia utekelezwaji wa sera , mikataba na maridhiano mbalimbali ya kimataifa na kikanda ambayo nchi yetu imetia saini kutekeleza haki za  binadamu."
 Mkurugenzi wa Shirika la Wazee Mkoa wa Morogoro , Samson Msemembo (katikati) akizungumza na waandishi habari juu kuelekea maadhimisho ya Siku ya haki za binadamu duniani ambayo hufanyika kila ifikapo Desemba 10 ya kila mwaka leo jijini Dar es Salaam , kushoto Katibu wa Mtandao wa Mashirika ya Wazee , Wilson Kaluwisa , kulia ni  Mjumbe wa Wazeee, Getrude Msangule.
 Katibu wa Mtandao wa Mashirika ya Wazee, Wilson Kaluwisa akizungumza juu utekelezaji  mikataba ya wazee katika masuala ya haki binandamu leo jijini Dar es Salaam.  

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...