Na.WAMJW-Rufiji.

Utekelezaji wa mpango wa malipo kwa ufanisi(RBF) Wilayani Rufiji umeleta mabadiliko makubwa katika Vituo vya afya na Zahanati kwa uboreshaji wa miundombinu pamoja na upatikanaji wa dawa muhimu

Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu  wakati alipotembelea Kituo cha Afya cha Ikwiriri na Zahanati ya Nyamwage katika ziara yake ya kuangalia utekelezaji unaofanyika kupitia mpango wa malipo kwa ufanisi unaotekelezwa katika mikoa nane nchini

Waziri Ummy alisema mabadiliko hayo katika sekta ya afya yamefanyika katika maeneo ya utoaji huduma,Uongozi na Utawala,Rasilimali watu,Mifumo ya usimamizi wa utoaji taarifa za afya,madawa na teknolojia ya afya ambapo mfumo huo umesaidia maboresho, uwajibikaji,ufanisi na usawa kwani dhana hiyo inamfanya mtoa huduma kulipwa kulingana na matokeo ya kazi yake ambayo amehakikiwa na hivyo kufanya vituo hivyo kuongeza hali ya upatikanaji wa dawa na kuboresha miundombinu ya vituo hivyo

"Tumeanza mpango huu katika mikoa 8,tumefanya tathimini kwenye vituo vya afya na zahanati zote za Mkoa wa Pwani ikiwemo Wilaya ya Rufiji,tukabaini vituo vya afya na zahanati hazikuwa na viwango vya ubora unaotakiwa, tukaona tuwapatie  shilingi milioni 10 kila kituo vilivyokidhi kwa ajili ya kuboresha miundombinu"alisema Waziri ummy.

Hata hivvyo aliipongeza kamati ya afya ya kijiji cha Nyamwage kwa kutumia ipasavyo shilingi milioni 10 kwa kuongeza urefu wa paa na kupaua,kuweka malumaru na kuongeza matundu ya choo pamoja na tundu moja la choo kwa ajili ya walemavu"nikupongeze mganga mfawidhi kwa kuboresha zahanati hii kwakweli unapaswa kupongezwa kwani umefanya vizuri ila badilika lugha chafu kwa wananchi haitakiwi,nakupa mwezi mmoja ila kwa upande huu mwingine umenifurahisa,mnyonge mnyongeni ila haki yake mpeni"

Mpango wa Malipo kwa Ufanisi waleta mabadiliko hayo ikiwemo ujenzi na ukarabati wa choo na jengo hilo,kama jengo lionekanavyo pichani juu na chini Waziri Ummy akikagua choo hicho.

Waziri Ummy Mwalimu akipokea mabango kutoka kwa wananchi yenye jumbe mbalimbali kuhusiana na changamoto za Afya, wakati alipokuwa akitembelea Kituo cha Afya cha Ikwiriri na Zahanati ya Nyamwage katika ziara yake ya kuangalia utekelezaji unaofanyika kupitia mpango wa malipo kwa ufanisi unaotekelezwa katika mikoa nane nchini. 
 Waziri wa Afy,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu  akimwelekeza mmoja wa Wazee waliopata vitambulisho vya Matibabu bure kwa Wazee wakati wa tukio hilo mapema leo Wilayani Rufiji.
  Waziri wa Afy,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu  akimkabidhi mmoja wa Wazee kitambulisho cha Matibabu bure kwa Wazee wakati wa tukio hilo mapema leo Wilayani Rufiji.
  Waziri wa Afy,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu  akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuwakabidhi baadhi ya Wazee vitambulisho vya Matibabu bure kwa Wazee alipokuwa akitembelea Kituo cha Afya cha Ikwiriri na Zahanati ya Nyamwage katika ziara yake ya kuangalia utekelezaji unaofanyika kupitia mpango wa malipo kwa ufanisi unaotekelezwa katika mikoa nane nchini. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...