Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii
Kampuni ya fuya Nicol imefungua kesi ya madai katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu dhidi ya aliyekuwa Mwenyekiti wa bodi ya Nicol, Felix Mosha na aliyekuwa Mtendaji Mkuu (CEO, Kathleen Armstrong.
Kesi hiyo ya madai namba 282 ya 2017 inasikilizwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Respius Mwijage, ambapo upande wa wadaiwa umetakiwa kupeleka utetezi wao,Desemba 20, 2017 na kesi hiyo imepangwa kutajwa Januari 24,2018.
Kwa mujibu wa kesi hiyo, upande wa wadai, wanaiomba mahakama hiyo, iamuru wadaiwa hao walipe kiasi cha Sh 180,096,097 kama gharama za hasara walizoingia.
Pia wanaomba mahakama iamuru warejeshe magari, walipe riba ya asilimia 26% pamoja na gharama za kesi.
Katika kesi hiyo, akina Mosha ambao ni wadaiwa wanatetewa na Wakili Hurbet Nyange huku Nicol ambaye ni mdai anawakilishwa na Wakili Benjamin Mwakagamba kutoka kampuni ya uwakili ya BM.
Kwa mujibu wa kesi hiyo inadaiwa kuwa Mosha pamoja na kuondolewa uenyekiti na wanahisa mnamo mwaka 2012, lakini bado ameshindwa kukabidhi gari la ofisi aina ya Landcruiser namba T 133 AVG ambapo ilipelekea ofisi ya Nicol kutafuta usafiri mwingine.
Kwa upande wa aliyekuwa Mtendaji Mkuu Kathleen Armstrong yeye anadaiwa kwamba akiwa amesimamishwa na baada ya kuondolewa na wanahisa, alishiriki katika kutapanya mali za Nicol ikiwamo kuuza gari aina ya Mitsubish Center Fuso bila idhini ya bodi ama Wanahisa .
Mahakama imeagiza mdaiwa wa pili katika kesi hiyo, Kathleen Armstrong ambaye ni raia wa Marekani apelekewe notisi kwa njia sahihi.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...