Naibu
Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo hapo jana alifanya ziara kwenye
machimbo ya Jasi (Gypsum) ya Mkoani Singida na kuzungumza na
Wafanyabiashara na Wachimbaji wa Madini hayo ambapo aliwahakikishia
ushirikiano wa dhati wa kufikia malengo waliyojiwekea.
Alitembelea
maeneo ya machimbo ya Madini ya Jasi na Viwanda vidogo vya uongezaji
thamani ya madini hayo ikiwemo viwanda vya kusaga madini ya Jasi ambayo
unga wake unasafirishwa nje ya Mkoa huo, viwanda vya kutengeneza chaki
vilivyopo Itigi na kiwanda cha utengenezaji wa mapambo ya majumbani
kilichopo Singida Mjini.
Naibu
Waziri Nyongo yupo Mkoani Singida kwenye ziara ya siku Tatu ya
kutembelea maeneo mbalimbali ya uchimbaji wa madini Mkoani humo ili
kujionea shughuli zinazofanywa kwenye maeneo hayo na kuzungumza na
wachimbaji wa madini ili kubaini changamoto zinazowakabili kwa lengo la
kutafuta ufumbuzi wake.
Kwa
mujibu wa wachimbaji wa madini hayo, Madini ya Jasi hutumika kwa
matumizi mbalimbali ikiwemo kutengenezea chaki, hospitalini kwa watu
waliovunjika na kutengeneza viungo bandia, kutumika kutengenezea saruji,
urembo majumbani, hutumika kama insulation kwenye majengo makubwa kwa
kuwa Jasi huzuia moto, kutengenezea midoli na masanamu, kutengeneza meno
bandia na pia hutumika kama mbolea
Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (kulia) akishuhudia upakiaji wa Madini ya Jasi katika kijiji cha Kihanju, Itigi yanayosafirishwa kuelekea kwenye Kiwanda cha Saruji cha Mbeya Cement ikiwa ni moja ya malighafi ya kutengenezea Saruji.
Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (kushoto) akiwasikiliza wachimbaji na wafanyakazi wa machimbo ya Jasi, yaliyopo katika Kijiji cha Kihanju, Itigi, Mkoani Singida alipofanya ziara kwenye machimbo hayo.
Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (wa pili kushoto) akitazama hatua ya uchomaji wa Madini ya Jasi kwenye kiwanda cha kampuni ya mzawa cha RSR kilichopo katika Kijiji cha Sanjaranda, Itigi kabla ya kusagwa kuwa unga na baadaye kusafirishwa hadi Dar es Salaam kwa ajili ya kuuzwa na mwingine kutumika katika Kiwanda cha kutengenezea mapambo ya Majumbani, katika kiwanda kilichopo Singida mjini.
Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo akitazama Chaki zinazozalishwa na Kiwanda cha Dobercolor kilichopo katika Kijiji cha Majengo, Itigi ambazo huuzwa ndani na nje ya Mkoa huo huku lengo likiwa ni kuuza nje ya Tanzania.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...