Na Woinde Shizza,Simanjiro.

Timu ya jamii ya wafugaji wa Naisinyai S. C ya Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, imeshinda ngao ya maadili iliyoandaliwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kwa kuifunga Mirerani SC kwa penalti 6-5.

Katika mchezo huo wa fainali uliochezwa juzi kwenye uwanja wa barafu mji mdogo wa Mirerani, mgeni rasmi alikuwa Katibu Tawala wa Wilaya hiyo Zuwena Omary. Hadi dakika 90 ya mchezo ulipomalizika timu hizo zilikuwa hazijafungana na walipopigiana penalti tano kwa tano hakukuwa na mshindi ndipo wakapigiana penalti moja kwa moja na Naisinyai ikashinda. 

Akizungumza wakati wa kukabidhi ngao hiyo ya maadili kwa timu ya Naisinyai,Katibu Tawala Omary alisema jamii inapaswa kupiga vita matumizi ya vitendo vya rushwa kwa kila sehemu. Alisema jamii inapaswa kuzingatia hilo kupitia kauli mbiu ya wajibika, piga vita rushwa, zingatia maadili, haki za binadamu na utawala bora kuelekea uchumi wa kati. 

"Tupige vita rushwa kila mahali, kuanzia michezo ni, makazini, polisi, hospitalini, mahakamani na kila eneo ukiona rushwa inatumika toeni taarifa," alisema Omary. Mkuu wa Takukuru wilaya ya Simanjiro Mashauri Elisante alisema mashindano hayo yalishirikisha timu nne za Naisinyai SC, Mirerani SC, Veterani Mirerani za Simanjiro na Tanzanite FC ya wilaya ya Arumeru mkoani Arusha. 

Alisema lengo la mashindano hayo ni maadhimisho ya siku ya maadili na haki za binadamu kitaifa na kupiga vita vitendo vya rushwa. Mwenyekiti wa Kijiji cha Naisinyai, Taiko Laizer alisema hii ni mara ya pili kwa mwaka huu timu hiyo kubeba ubingwa wa soka kwani awali walishinda kombe la mbunge wa jimbo la Simanjiro James Ole Millya. 
Laizer alisema siri ya ushindi mara mbili kwa mwaka mmoja kwenye timu hiyo ni kuzingatia mazoezi, nidhamu na ushirikiano wa uongozi na wananchi kwa ujumla. 
Mwenyekiti wa Kijiji cha Naisinyai Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, Taiko Laizer akimbeba golikipa wa Naisinyai SC Joseph John baada ya kunyakua ngao ya Takukuru kwa kuifunga Mirerani SC kwa penalti 6-5
Mwenyekiti wa Kijiji cha Naisinyai Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, Taiko Laizer akimbeba golikipa wa Naisinyai SC Joseph John baada ya kunyakua ngao ya Takukuru kwa kuifunga Mirerani SC kwa penalti 6-5

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...