Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Mama Anne Makinda akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa siku moja na Watoa Huduma wake wa Mkoa wa Dar es Salaam kwa lengo la kupeana mrejesho wa huduma kwa wanachama, uliofanyika kwenye Ukumbi wa GEPF, jijini Dar es salaam leo.

Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), umekutana na Watoa Huduma wake wa Mkoa wa Dar es Salaam kwa lengo la kupeana mrejesho wa huduma kwa wanachama lakini pia kujadili mambo mbalimbali yatayofanikisha kuboresha huduma za matibabu.

Kikao hicho kimefanyika leo, Dar es Salaam kikiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya NHIF, Mama Anne Makinda ambaye amewataka watoa huduma kuhakikisha wanawahudumia vizuri wanachama wa Mfuko ili kuondokana na malalamiko yasiyo ya lazıma.

“Wanachama wetu wanapofika huko kwenu wahudumieni vizuri ili waone thamani ya fedora zao walizochangia lakini pia waone umuhimu wa kuendelea kuwa wanachama….tambueni mdomo ni sumu kubwa hakikisheni mnautumia vizuri” alisema Mama Anne Makinda.

Kwa  upande wa wagon huduma ambar waliwakilishwa na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Grace Magembe, aliupongeza Mfuko kwa jitihada mbalimbali ambazo umekuwa ukifanya kuhakikisha huduma za afya zinaboreshwa na wanachama wanahudumiwa kwa kiwango kikubwa.
 Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Bernard Konga akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa siku moja na Watoa Huduma wake wa Mkoa wa Dar es Salaam kwa lengo la kupeana mrejesho wa huduma kwa wanachama, uliofanyika kwenye Ukumbi wa GEPF, jijini Dar es salaam leo.
 Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Grace Magembe akitoa salamu za watoa huduma katika mkutano huo.
 Kaimu Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Angela Mziray akitoa muongozo wa Mkutano huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...