Afisa Mkuu wa Fedha wa Benki ya Exim Tanzania, Selemani Ponda na Mkurugenzi wa Mikakati wa kampuni ya Selcom, Benjamin Mpamo wakizindua Cashpoint ATM ambayo itawawezesha watumiaji wamobile money, Visa na Master Card wa ndani ya nchi na wa kimataifa kutoa fedha kwa kutumia kadi au bila kutumia kadi.

KATIKA kuendelea kuboresha huduma za kifedha kwa watanzania, Benki ya Exim Tanzania kwa kushirikiana na Selcom imezindua rasmi Cashpoint ATM zinazowawezesha wateja wa Selcom, Exim benki watumiaji wa mobile money, Visa na Master Card wa ndani ya nchi na wa kimataifa kutoa fedha kwa kutumia kadi au bila kutumia kadi.

Huduma hii inawawezesha wateja wa Tigo Pesa, M-pesa, Airtel Money, Selcom Card, Halopesa na wateja wanaotumia huduma za kibenki kwa njia ya simu kutoa fedha kwa njia ya token. Mteja atatumia simu yake kutoa fedha na kisha kuingiza token namba atakazopkea kwenye ATM, namba ya simu na kiasi anachohitaji kutoa na kufanikiwa kutoa fedha bila kutumia kadi. Kwa wateja wa Visa Card na Master Card, wao wanaweza kutoa fedha lakini kwa kutumia kadi zao kupitia Cashpoint ATM yoyote kwa urahisi zaidi.
“Tukiwa kama benki ya nne inayoongoza Tanzania katika mali, tungependa kusisitiza kujitolea kwetu katika kutengeneza mazingira ambayo huduma za kibenki zinapatikana kwa urahisi.” Ushirikiano huu utaokoa watumiaji wengi kwa kuwa wanaweza kutumia ATM moja na inaruhusu matumizi bila kadi.

Ubunifu ni ahadi tunayowapa wateja wetu. Benki imepata mafanikio makubwa kwenye uvumbuzi wa teknolojia yenye kwango cha dunia na bidhaa zinazolenga wateja. Tunajivunia kuwa benki ya kwanza nchini Tanzania kuanzisha kadi za Mikopo, Hati fungani za kubadilisha biashara, na Taasisi ya mafunzo ndani ya benki iliyothibitishwa na ISO. Sisi pia tulitoa ufumbuzi wa vituo rununu vya kutolea fedha (ATM), Huduma ya maasaa 24 kila siku katika matawi kadhaa yenye kuweka hela na mpango wa kipekee wa fedha kwa wanawake nchini Tanzania. Benki ya Exim ni benki inayongezeka kwa haraka yenye ubunifu wa kidigitali ambayo ina bidhaa nyingi na huduma za kuvutia zaidi zilizozinduliwa mwaka 2017 kama kadi zaa benki za kusafiri, Kadi ya benki ya mshahara kabla ya kulipwa, Kadi ya benki ya dola za Kimarekani na huduma za benki kwenye simu.

Hapo awali kumekuwa na changamoto kubwa katika utoaji wa fedha, na kwa kupitia mfumo huu mpya wa Selcom Cashpoint ATM sasa wateja wataweza kuepuka kero na vikwazo mbalimbali walivyokuwa wakikutana navyo hapo kabla na kufanya miamala hiyo kwa haraka, urahisi na salama zaidi. Kwenye ushirikiano huu Selcom hutoa usimamizi wa vifaa wakati Benki ya Exim hutoa usimamizi wa fedha, leseni ya benki ya kuendesha ATM pamoja na MasterCard / Visa ili kuwezesha wateja kupata huduma za utoaji wa fedha kwa njia ya haraka, rahisi na salama.

Mkurugenzi wa mikakati, Benjamin Mpamo kutoka Selcom aliongezea kwa ksuema, “Dhamira kuu ya Selcom ni kuwarahisishia maisha watanzania kwa njia ya teknolojia na kuhakikisha huduma za kifedha zinapatikana kwa njia rahisi na haraka kwa watanzania wote. Katika kuhakikisha tunatimiza dhamira hiyo, Selcom kwa kushirikiana na Exim Bank tumewaletea huduma hii mpya ya Cashpoint ATM ili kuwawezesha watanzania kutoa fedha kiurahisi kabisa muda wowote inapohitajika”.

Huduma zingine zitakazopatikana kwenye Cashpoint ATM hivi karibu ni pamoja na kununua LUKU, kulipia bili ya maji (Dawasco), kununua muda wa maongezi, kuangalia salio na kupata taarifa fupi ya miamala ya kadi kwa wateja wa Visa Card na Master Card.

Lengo kuu la Cashpoint ATM ni kuwarahisishia wananchi huduma za kutoa fedha na kuwawezesha kutoa fedha muda wowote kwa haraka, salama na uhakika bila kuwa na wasiwasi wa kukosa huduma hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...