Wanafunzi
watano wa shule za Msingi za serikali hapa nchini wameshinda shindano
la uchoraji la “Ishi Huru” ambalo liliandaliwa na Kampuni ya The Jubilee
Insurance Company of Tanzania Limited na Jubilee Life Insurance
Corporation of Tanzania Limited. Walioshinda wamepewa zawadi za bima za
Elimu za jubilee Life insurance, yaani “Jubilee Career Life Cover”
watakayoipata watakapoingia elimu ya sekondari.
Shindano hilo liliendeshwa nchi nzima kwa kupitia TAMISEMI ambapo wanafunzi watano wameibuka kidedea baada ya kuchora na kutuma picha hizo.
Director of Surveillance and prudential supervision wa Mamlaka ya usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA), Mr. Elia Kajiba ameishukuru Jubilee Insurance kwa kuendesha shindano hilo ambalo limeweza kuwapa zawadi wanafunzi watano ya kuwa na uhakika wa kugaramiwa katika elimu yao ya sekondari.
Amesema kuwa waendelee kuandaa mashindano na vitu mbalimbali ambavyo vitainufaisha jamii na kuwasukuma wanafunzi kushiriki.
Nae Mwenyekiti wa bodi ya Jubilee Life Insurance Corporation of Tanzania Limited ambaye pia ni Mwenyekiti msaidizi wa bodi ya The Jubilee Insurance Company of Tanzania Limited, Mr. Shabir Abji amesema kuwa katika kuadhimisha miaka 80 tangu kuanzishwa kwa Kampuni ya Jubilee Insurance , uongozi wa kampuni hiyo iliamua kuishirikisha jamii katika kusheherekea na kutoa huduma mbalimbali kwa jamii kama zawadi hizi kwa wanafunzi walioshinda shindano la uchoraji, kujenga na kuboresha vyoo vya shule za msingi nane hapa nchini, kujenga nyumba za walimu na madarasa ya shule kadhaa hapa nchini.
Mzazi wa Joseph Mwakyembe wa Mbozi mkoani Songwe, Joyce Mbuya amesema kuwa, anayo furaha kubwa sana kwani mtoto wake amemuwezesha yeyekufika Dar es Salaam na kupokea zawadi ambayo itamuhakikishia elimu yake ya Sekondari kutoka Jubilee Insurance.
Amesema kuwa Jubilee Insurance imekuwa ya kwanza kuwafikia wananchi wa kawaida kwa kutafuta vipaji vya wanafunzi.

Mwenyekiti
wa bodi ya Jubilee Life Insurance Corporation of Tanzania Limited
ambaye pia ni Mwenyekiti msaidizi wa bodi ya The Jubilee Insurance
Company of Tanzania Limited, Mr. Shabir Abji , akizungumza na wageni
waalikwa kwenye utoaji wa zawadi kwa wanafunzi wa shule za msingi
walioshinda kwenye shindano la uchoraji la “ Ishi Huru” la Kampuni ya
Jubilee Insurance lililofanyika hapa nchini.
Mgeni
rasmi Director of Surveillance and prudential supervision wa Mamlaka
ya usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA), Mr. Elia Kajiba akitoa shukrani
kwa Kampuni ya Jubilee Insurance kwa kuihudumia jamii pamoja na
kuwasisitiza waendelee kujikita hasa kwenye kaya zenye kipato cha chini
ili kuinua jamii.
Mkuu wa Kitengo cha Fedha Jubilee Life Insurance Corporation of
Tanzania Limited, Helena Mzena akitoa historia ya shindano
lililoshirikisha shule za msingi hapa nchini kwa wanafunzi wa darasa la
Tatu , katika sherehe za ugawaji wa zawadi kwa wanafunzi watano
walioshinda.
Chief
Executive Officer wa kampuni ya The Jubilee Insurance Company of
Tanzania, Mr. Dipankar Acharya akizungumza ujumbe mfupi katika sherehe
zautoaji wa zawadi kwa wanafunzi wa shule za msingi waliofanya vizuri
kwenye shindano la uchoraji la “Ishi Huru”.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...