Na Mwandishi Wetu
MKOA wa Dar es Salaam umeipatia Ngao Maalum shule ya St. Anne Maria kama sehemu ya kutambua mchango wake katika kuinua elimu hapa nchini.

Sherehe ya kuzawadia shule zilizofanya vizuri ilifanyika mwishoni mwa wiki ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam, Thelesia Mbando, kwenye kilele cha siku ya elimu Dar es Salaam, zilizofanyika ukumbi wa PTA Sabasaba.

Shule hiyo ilipewa ngao inayoonyesha kuwa ni miongoni mwa shule zilizofanya vizuri zaidi kwenye matokeo ya darasa la saba mwaka 2016, Best Performing Primary School in Tanzania.

Akizungumza mara baada ya kupokea ngao hiyo, Mkuu wa Shule hiyo, Gladius Ndyetabura alisema ngao hiyo imewapa changamoto ya kuendelea kufundisha kwa bidii ili hatimaye wapate matokeo mazuri zaidi ya mwaka huu.

Alisema ingawa shule yake imefanikiwa kuingia kumi bora kwenye matokeo ya darasa la saba mwaka huu, lakini hawajabweteka na badala yake wanafanya jitihada za kuwa namba moja.

“Kwenye matokeo ya darasa la saba mwaka huu tumefanikiwa kuwa wa kwanza Wilaya ya Ubungo, tumekuwa wa pili Mkoa wa Dar es Salaam na tumekuwa wanane kitaifa sasa hii haitufanyi tubweteke tutapambana kupata nafasi za juu zaidi,” alisema  

Aliushukuru uongozi wa Mkoa wa Dar es Salaam kwa kuwapa ngao hiyo ambayo imewapa motisha na ari ya kuendelea kufundisha kwa bidiii ili kupata matokeo mazuri zaidi ya waliyopata mwaka huu.

“Shule ni nyingi na ushindani ni mkubwa sana hivyo bado tunakazi ya kufanya kuhakikisha tunaendelea kuwa kumi bora na hata kuwa wa kwanza kitaifa, ingawa shule ni nyingi sana hapa Dar es Salaam lakini tuliopewa ngao na vyeti ni wachache sana sasa hii inaonyesha namna gani mchango wetu unavyothaminiwa,” alisema
Mwalimu Mkuu wa Shule ya St Anne Maria ya Mbezi kwa Msuguri, Gladius Ndyetabura akifurahia pamoja na wanafunzi wa shule hiyo ngao ambayo shule hiyo imepewa na Mkoa wa Dar es Salaam kuipongeza kwa kufanikiwa kuwa ya nane kitaifa na ya kwanza Wilaya ya Ubungo kwenye matokeo ya darasa la saba.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...