Mkuu wa Kanda ya Mashariki ya Kati na Africa wa kampuni ya World Remit, Andrew Stewart
akizungumza jambo katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es
Salaam kutangaza ushirikiano baina ya kampuni yake na Tigo Tanzania
unaowezesha Watanzania walioko nje ya nchi kutuma pesa kwa simu zao za
mkononi kwenda kwa huduma ya Tigo Pesa. Kushoto ni Afisa Mkuu wa Huduma
za Kifedha wa Tigo, Hussein Sayed.
Afisa Mkuu wa Huduma za Kifedha za Simu za Mkononi wa Kampuni
ya Tigo Tanzania, Hussein Sayed akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es
Salaam kutangaza ushirikiano baina ya kampuni yake na Tigo Tanzania
unaowezesha Watanzania walioko nje ya nchi kutuma pesa kwa simu zao za
mkononi kwenda kwa huduma ya Tigo Pesa. Kulia ni Mkuu wa Kanda ya Mashariki ya Kati na Africa wa kampuni ya World Remit, Andrew Stewart.
Meneja
Uhusiano wa Tigo Tanzania, Woinde Shisael akifafanua jambo katika
mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kutangaza
ushirikiano baina ya kampuni ya Tigo na ile ya World Remit unaowezesha
Watanzania walioko nje ya nchi kutuma pesa kwa simu zao za mkononi
kwenda Tigo Pesa. Kulia ni Afisa Mkuu wa Huduma za Kifedha wa Tigo,
Hussein Sayed na Andrew Stewart, Mkuu wa Kanda ya Mashariki ya Kati na
Africa wa kampuni ya World Remit .
WorldRemit na Kampuni ya kidigitali Tigo Tanzania wameshuhudia ukuaji wa
kasi wa huduma za kuhamisha fedha kwenda katika akaunti za fedha za simu za mkononi
nchini Tanzania, taarifa zimebainisha.
Katika kipindi cha miaka miwili cha ushirikiano baina ya kampuni hizi, huduma ya Tigo
imebainika kuwa ndiyo huduma ya kutuma fedha inayokuwa kwa kasi zaidi miongoni mwa
washirika wa WorldRemit.
Huduma hii inawawezesha Watanzania katika zaidi ya nchi 50 kutuma fedha kwenda katika
akaunti za fedha za simu za mikononi kwa haraka. Wamiliki wa akaunti za fedha za simu za
mkononi pia wanakuwa na uwezo wa kutuma fedha ndani ya nchi, kununua muda wa
maongezi, kulipia ankara au kutoa fedha taslimu kupitia mtandao mkubwa wa mawakala wa
Tigo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...