Na Mwandishi Maalum,

Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Biswalo Magaga,(DPP) amesema , utekelezaji wa mpango wa Serikali wa kutengenisha jukumu la upepelezi na upelelezi mashataka umekuwa wa mafanikio makubwa yakiwamo yakupunguza mlundikano wa mahabusu.

Mkurugenzi wa Mashtaka ameyasema hayo wakati alipokuwa akielezea utekelezaji wa mpango huo tangu ulipoanzishwa kwa sheria ya mfumo wa mashtaka 2007,mbele ya wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali linalokutana kwa siku mbili mkoani Dodoma.

“ Tangu kuanza kwa mpango huu tumepata mafanikio makubwa, kwani kwa sasa kumekuwa na wafungwa wengi kuliko mahabusu kwa maana kwamba idadi ya mahabusu imezidi kwa 2000 kama ilivyo kuwa huko nyuma ”. Akabainisha Mkurugenzi wa Mashtaka.Mpango wa serikali wa kutenganisha shughuli za upelelezi na mashtaka ulilenga kuondoa tatizo la haki kuchelewa kutendekea na kesi kuchukua muda mrefu mahakamani kwa sababu ya muda mrefu unaotumika katika upelelezi.

Mafanikio mengine kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Mashtaka ni jamii kurejesha imani kwa vyombo vya sheria kutokana na haki kutendeka na kwa wakati na hivyo kupunguza vitendo vya wananchi kujichukulia hatua mkononi.Mafanikio mengine kesi zinazoendeshwa na Mawakili wa Serikali zimekuwa na mafanikio makubwa ikilinganishwa na zile ambazo zinasimamiwa na mawakili wakujitegemea. Kiasi cha kusababisha kupunfua kwa ukataji wa rufaa na mashauri ya jinani kupugua kutokana na jamii kutambua uhalifu haulipi.

“ Kutokana na utekelezaji wa mpango huu, siyo tu kumepunguza rufani zinazopelekwa Mahakama ya Rufaa kwa wakata rufaa kupungua kutokana na weledi wa mawakili na kazi kubwa na nzuri wanayoifanya ya kuiwakilisha serikali Mahakamani”.Amebainisha Mkurugenzi wa Mashtaka.

Akaongeza pia kwamba hata barua za malalamiko kutoka kwa wananchi zimepungua kiasi kwamba mafaili hayajai tena barua za malalamikio kama ilivyokuwa huko nyuma na hiki ni nikielelezo kikubwa kwamba wananchi wanapata huduma za kisheria kwa ufanisi mkubwa” akasisitiza Mkurugenzi wa Mashtaka. 

Pamoja na mafanikio hayo, Mkurugenzi wa Mashtaka ameelezea baadhi ya changamoto ni kutokuwapo kwa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika baadhi ya Wilaya hususani katika baadhi ya Wilaya ambazo zinamtukio mengi ya jinai.Amesema ufinyu wa bajeti na upungufu wa raslimali watu ndiyo unaochangia au kurudisha nyuma kasi ya ufunguzi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu kila wilaya ili kuwafikishia huduma kwa karibu wananchi.

Katika hatua nyingine, Mkurugenzi wa Mashtaka ametoa rai kwa Mawakili Wafawidhi pamoja na Mawakili wote kutekeleza majukumu yao ya kuisimamia Serikali bila woga na kwa kuzingatia maadili na weledi na wasikubali kuyumbishwa.“Tekelezeni majukumu yenu kwa mujibu wa taaluma yenu, msiogope kusimamia ukweli na kile mnachokiamini katika utekelezaji wa majukumu yenu”. Akasisitiza Mkurugenzi wa Mashtaka.
Mkurugenzi wa Mashtaka ( DPP) Bw. Biswalo Magaga akiwaeleza wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu namna utekelezaji wa utenganishaji wa shughuli za uendeshaji mashtaka na upelelezi unavyoleta tija na mafanikio yakiwamo ya kupunguza msongamano wa mahabusu magerezani. wengine katika picha ni Mwenyekiti wa Baraza la wafanyakazi, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. George Masaju, Makamu Mwenyekiti, Bw, Gerson Mdemu na Katibu Msaidizi wa Baraza, Bw. Michael Masanja
Wakili wa Serikali Mwandamizi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mkoa wa Mwanza, Revinna Tibilengwa akichangia majadiliano kuhusu utekelezaji wa utenganishaji wa shughuli za mashtaka na upelelezi
Wakili Mfawidhi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu Mkoa wa Ruvuma, Bw. Renatus Mkude, akiwasilisha taarifa kwa niaba ya Mawakili Wafawidhi wa Mikoa na Wilaya ambako zipo Ofisi za Mwanasheria Mkuu wa Serikali mbele ya wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...