Na Woinde Shizza,Arusha
Jumla ya Shilingi milioni 605 zimetolewa kama mkopo wa kuwanufaisha wajasiriamali walioko kwenye vikundi vya kinamama na vijana pamoja na walemavu waliopo  katika Halmashauri ya Jiji la Arusha.
Akizungumzia mikopo hiyo inayotolewa na Halmashauri Afisa Ustawi wa Jamii Jiji la Arusha Hanifa Ramadhani amesema kuwa mikopo hiyo inatolewa ili kuwawezesha kinamama na vijana kuondokana na hali ngumu za kiuchumi zinazowakabili ili kuinua uchumi .
Mkuu wa Wilaya ya Arusha Gabriel Daqarro amewataka Vijana ambao ni wasomi kujiunga katika vikundi hivyo na kupata mikopo ili kujiendeleza kiuchumi badala ya kusubiri ajira serikalini ile hali nafasi ni chache na wahitimu wa vyuo ni wengi.
Kwa upande wao Wanufaika wa Mikopo hiyo kwaniaba ya Walemavu Mwajuma Juma  na Patrick Petro  wameishukuru serikali kwa kutoa mikopo hiyo yenye masharti nafuu ambayo itawasaidia kujikwamua kiuchumi.
Mkuu wa Wilayaya Arusha  Gabriel Daqarro akabidhi hundi ya shilingi milioni 500 ya mkopo wa kinamama iliyotolewa na Halmashauriya Jiji la Arusha 

 Kinamama na vijana waliokusanyika katika ukumbiwa Arusha School kupewa mafunzo kabla y akupatiwa mikopo ya halmashauri ya jiji la Arusha.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...