Na Hamza Temba, Mbarali - Mbeya
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga ametoa miezi mitatu kwa uongozi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania TAWA kukamilisha malipo ya fidia ya shilingi milioni 771.6 kwa kaya 308 za Kitongoji cha Machimbo ili ziweze kupisha eneo la hifadhi katika Pori la Akiba la Mpanga Kipengele.
Naibu Waziri Hasunga ametoa agizo hilo jana katika mkutano wa hadhara baada kutembelea kitongoji hicho katika Wilaya ya Mbarali Mkoani Mbeya wakati wa ziara yake ya kikazi kwa ajili ya kutatua migogoro kwenye maeneo ya hifadhi mkoani humo.
“Kaimu Mkurugenzi (TAWA) kama unavyoona wananchi hawa wapo tayari kupisha eneo hili la hifadhi, wanachosubiri ni malipo yao ya fidia, naagiza mpaka ifikapo mwezi Februari mwakani (2018) wawe wameshalipwa fidia zao, na ikiwezekana hata ndani ya mwezi Januari wawe wameshalipwa,”alisema Hasunga.
Awali akiwasilisha taarifa ya pori hilo, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo, David Kenyata alisema wakati pori hilo linaanzishwa mwaka 2002 kwa Tangazo la Serikali Na. 483 wananchi wa kitongoji hicho na vitongoji vingine walikuwa ndani ya eneo hilo la hifadhi.
Alisema mazungumzo yalishafanywa kupitia vikao halali vya uongozi wa viijiji na halmashauri ambapo wananchi hao waliridhia kulipwa fidia ili kuachia maeneo hayo ya hifadhi.
Alisema sababu kubwa ya kuanzishwa kwa pori hilo ni pamoja na kuhifadhi vyanzo vya maji yanayotiririka kwenda mto Ruaha na kwenye mabwawa ya kidatu na mtera yanayotumika kuzalisha umeme nchini.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (waliokaa mbele katikati) akizungumza na watumishi wa Pori la Akiba Mpanga Kipengele alipotembelea makao makuu ya pori hilo jana katika Wilaya ya Wangin'ombe mkoani Njombe.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (wa pili kushoto) akisalimiana na Kaimu Meneja wa Pori la Akiba la Mpanga Kipengele, Stanslaus Odhiambo muda mfupi baada ya kuwasili makao makuu ya pori hilo jana katika Wilaya ya Wanging'ombe mkoani Njombe.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga akizungumza na wananchi wa Kitongoji cha Machimbo wapatao kaya 308 katika Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya jana ambapo aliiagiza Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania kuwalipa fidia ya shilingi milioni 771.6  kabla ya Februari, 2018 ili wapishe eneo la Hifadhi katika Pori la Akiba la Mpanga Kipengele.
Baadhi ya wananchi wa kitongoji cha Machimbo wapatao kaya 308 katika Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya wakimsikiliza Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga ambaye aliwatembelea jana na kuagiza Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania iwalipe fidia ya shilingi milioni 771.6 kabla ya Februari, 2018 ili wapishe eneo la Hifadhi katika Pori la Akiba la Mpanga Kipengele alipowatembelea.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (kulia) akizungumza na wananchi wanaojishughulisha na kilimo cha umwagiliaji katika Skimu ya Igomelo, wilaya ya Mbarali Mkoani Mbeya ambao waligomea zoezi la uwekwaji wa vigingi vya mpaka kwenye eneo lao na Pori la Akiba la Mpanga Kipengele kwa hofu ya kupoteza maeneo hayo. Baada ya kuwaelimisha wananchi hao walikubali kutoa ushirikiano kwa mamlaka husika ili kukamilisha zoezi hilo. Taarifa kamili BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...