Na Rhoda Ezekiel Kigoma.

WAKULIMA wa Sikimu ya Umwagiliaji ya Mpunga Katika vijiji vya Katengera na Ruhiti Wilayani Kakonko, wametakiwa kuongeza ufanisi kwa zao la Mpunga ilikuzalisha mazao ya kutosha kutokana na zao hilo kuwa zao la biashara kwa Wilaya hiyo na serikali kwa kushirikiana na wawekezaji wamewekeza fedha nyingi ilikuinua uchumi wa Wananchi hao.

Wito huo ulitolewa na Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagala, wakati akikabidhi vifaa vya upaliliaji kwa kikundi cha upaliliaji vyenye thamani ya shilini 12,700,000 vilivyo tolewa na shirika LINK vitakavyotumika Kupalilia Katika Mashamba ya Mpunga katika sikimu ya Katengera na Ruhiti lengo ikiwa ni kuwaongezea kipato Wanawake wanaojishughulisha na upaliliaji pamoja na wakulima wa mpunga kwa kuongeza uzalishaji.

Mkuu huyo aliwaagiza wakulima hao kuongeza uzalishaji kutokana na serikali kwa kushirikiana na Wafadhiri wametatua changamoto ya vifaa vya kupalilia vilivyo kuwa vikisababisha kupata mazao machache na kuwataka kulima misimu miwili na kila hekali moja kuzalisha gunia 40 hadi 45 tofauti na kipindi ambacho walikuwa hawana nyenzo hizo.

" niwaombe wakulima wote kulima marambili katika sikimu hii sikimu hii ni ya umwagiliaji kwahiyo maana ya kumwagilia lazima mlime na kiangazi, serikali imeweka fedha nyingi sana katika sikimu hii lazima mjitahidi kuzalisha ilituweze kupata viwanda vya kukoboa mpunga na kuinua uchumi wa wanakakonko kwa yeyote atakae shindwa kulima marambili tutachukua shamba lake na tuwagawie wawekezaji iliwaweze kuwekeza zaidi na kupata mazao ya kutosha", alisema Ndagala.

Hata hivyo Ndagala aliwaagiza Wakulima hao kuzingatia maelekezo ya mabwana shamba katika uwekaji wa mbolea, pamoja na kuzingatia Muda wa kupalilia ilimuweza kuongeza uzalishaji na kupata mazao yenye ubora.
 Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagala akishiriki kupalilia zao la Mpunga katika shamba la WAKULIMA wa Sikimu ya Umwagiliaji ya Mpunga Katika vijiji vya Katengera na Ruhiti Wilayani Kakonko
  Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagala akikabidhi vifaa vya upaliliaji kwa kikundi cha upaliliaji vyenye thamani ya shilini 12,700,000 vilivyo tolewa na shirika LINK vitakavyotumika Kupalilia Katika Mashamba ya Mpunga katika sikimu ya Katengera na Ruhiti lengo ikiwa ni kuwaongezea kipato Wanawake wanaojishughulisha na upaliliaji pamoja na wakulima wa mpunga kwa kuongeza uzalishaji.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...