Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na Taasisi ya Okoa Moyo wa Mtoto (Save a Child’s  Heart – SACH) ya nchini Israel zimewapeleka  watoto sita (6) wenye umri wa mwaka mmoja hadi  miaka kumi na tatu  nchini Israel kwa ajili ya matibabu ya moyo.

Katika safari yao ya matibabu nchini humo watoto, wauguzi pamoja na wazazi wao wameondoka alfajiri ya jana tarehe  10/12/12. Baada ya matibabu ya watoto kukamilika  Maafisa Wauguzi wawili watabaki kwa ajili ya kuhudhuria mafunzo ya mwaka mmoja ya jinsi ya kuwahudumia wagonjwa waliopo katika wodi ya uangalizi maalum (ICU) na chumba cha upasuaji.

Taasisi  yetu inatibu magonjwa mbalimbali ya moyo kwa watoto  kupitia  wataalamu wazalendo tulionao. Hata hivyo tunamkataba na Israel kwa baadhi ya wagonjwa wachache wanaohitaji utaalamu wa juu zaidi kuwapeleka nchini humo kwa ajili ya matibabu.

Tunaushirikiano mzuri na nchi ya Israel kwani gharama za matibabu ya watoto hawa zinagharamiwa na SACH. Licha ya Maafisa Wauguzi wawili kubaki nchini humo kwa ajili ya kuhudhuria mafunzo pia tuna madaktari bingwa wa magonjwa ya moyo sita   na wauguzi wawili ambao wamesoma nchini Israel na hivi sasa wanatibu wagonjwa katika Taasisi yetu.Aidha Daktari wetu mmoja bado anaendelea na masomo nchini humo.

Hili ni kundi la tano  la watoto kwenda kutibiwa magonjwa ya moyo nchini Israel tangu mwaka 2015 ambapo Taasisi ya Moyo ilianza ushirikiano  na Taasisi ya Okoa Moyo wa Mtoto (Save a Child’s Heart –SACH)  ya kuwapeleka wagonjwa nchini humo. Hadi sasa watoto 46 wameshatibiwa nchini humo na wanaendelea vizuri.

Taasisi inaendelea kutoa wito kwa wazazi na walezi wasisahau kupima afya za watoto wao pale watakapoona kuna hali ya tofauti katika ukuaji wa mtoto kwani magonjwa mengi ya moyo yanaanzia utotoni. Mtoto akianza kuuguwa magonjwa ya moyo wazazi wengi wanadhani ni matatizo ya kifua baada ya kumfikisha mtoto Hospitali na kufanyiwa vipimo  ndipo inagundulikwa kuwa mtoto anasumbuliwa na magonjwa ya moyo.

Imetolewa na :

Kitengo cha Uhusiano na Masoko
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete
11/12/2017.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...