MKE wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa amewaomba wazazi wa wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi wahakikishe wanatumia sehemu ya kipato chao katika kuwekeza kwenye elimu ya watoto wao. Amesema elimu ndiyo jambo pekee linaoweza kumsaidia mtoto katika kutimiza ndoto zake za maisha pamoja na kumtoa katika kundi la wategemezi. 
Mama Mary aliyasema hayo jana (Jumamosi, Desemba 2, 2017), katika maafali ya shule ya awali na msingi ya Wonder Kids, iliyopo wilayani Ruangwa, Lindi. Mke wa Waziri Mkuu alialikwa katika maafali hayo kama mdau wa elimu. Maafali hayo yaliyohusisha watoto wa awali ambao wanaingia darasa la kwanza. 
 “Walimu wanafanya kazi kubwa ya kuhakikisha wanafunzi hao wanajua kusoma vizuri, hivyo wazazi watumie kipato chao kuwekeza katika elimu kwani faida watakuja kuiona baadaye.” Alisema kitaaluma yeye ni mwalimu hivyo anatambua kuwa walimu wanafanya kazi kubwa ya kuhakikisha wanafunzi hao wanajua kusoma vizuri na wanakuwa na tabia nzuri, hivyo wazazi hawana budi kushirikiana nao. Pia Mama Mary alitumia fursa hiyo kuwaomba wazazi wawatie moyo walimu kwa sababu kazi wanayoifanya ni kubwa. 
“Wote ni mashahidi watoto wetu tulivyowaleta na sasa ni tofauti.” Alisema ni vizuri wazazi wakashiriki kikamilifu katika suala la elimu kwa watoto wao ikiwa ni pamoja na kufuatilia maendeleo ya masomo yao badala ya kuwaachia walimu peke yao. 
 Kwa upande wake ,mgeni rasmi katika maafali hayo ambaye ni Muwakilishi Mkazi wa Children in Crossifire Bw Craig Ferla aliwapongeza wanafunzi hao kwa kutimiza moja ya hatua katika safari yao ya elimu na aliwasihi waendele kupenda kwenda shule na kusoma kwa bidii. Pia aliwapongeza wazazi kwa kutambua umuhimu wa elimu ya awali na kuwapeleka watoto wao kwenye shule hiyo ya Wonder Kids. 
“Wonder Kids ni mahali sahihi ambapo mtoto anapata elimu na malezi bora. Alisema elimu ya awali ninzuri kwa mtoto kwa kuwa inawawezesha kujua kusoma, kuandika na kuhesabu, hivyo aliwaeleza Wanaruangwa kutumia vizuri fursa ya uwepo wa shule hiyo katika wilaya yao. 
 Naye Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Bibi Nancy Tausi alisema Wonder Kid ilianzishwa Januari, 2017 ikiwa na wanafunzi 117 ambao ni wa kuanzia darasa la awali hadi darasa la tatu. Alisema lengo la kuanzisha shule hiyo ni kuhakikisha watoto wanapata kujua kusoma vizuri na kwamba wanatarajia kuanzisha darasa la kompyuta kwa ajili ya watoto kujifunza TEHAMA pamoja na kuanza kufundisha lugha ya Kifaransa.

 Watoto wa Shule ya Msingi na Awali ya Wonder Kids wakiimba wimbo wa Shule yao katika Mahafali ya Kwanza ya Shule hiyo iliyopo Ruangwa Mjini

 Wahitimu wa  darasa la Awali wa Shule ya Wonder Kids  wakiimba  katika Mahafali ya Kwanza ya Shulel hiyo iliyopo Ruangwa Mjini Desemba 2, 2017.
 Wahitimu wa  wa Shule ya Msingi na Awali ya Wonder Kids wakicheza ngoma ya asili  katika Mahafali ya Kwanza ya Shulel hiyo iliyopo Ruangwa Mjini 
 Mgeni Rasmi katika Mahafali ya kwanza ya Shule ya Awali na Msingi ya Wonder Kids ya mjini Ruangwa , Bw. Craig Ferla ambaye pia ni Mkurugenzi Mkazi wa Taasisi ya Children in Crossfire akimkabidhi cheti  kwa mhitimu wa Mafunzo ya Awali katika shule hiyo, Jasmine Madamba, Desemba 2, 2017.Wapili kuil ni Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa.
Sehemu ya wazazi na waalikwa wa Mahafali ya Kwanza ya Shule ya Awali na Msingi ya Wonder Kids ya Mjini Ruangwa wakimsikiliza Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa wakati alipozungumza katika Mahafali hayo

Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa akizungumza katika mahafali ya kwanza ya Shule ya Awali na Msingi ya Wonder Kids ya Mini Ruangwa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...