NA K-VIS BLOG/Khalfan Said

WAZIRI wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Isack Kamwele, ameanza ziara ya siku mbili ya kukagua baadhi ya miradi inayosimamiwa na Mamlaka ya Maji  Safi na Maji Taka, (DAWASA), jijini Dar es Salaam, Desemba 5, 2017.
Katika siku yake ya kwanza ya ziara hiyo, Waziri alitembelea Mradi wa Uboreshaji Mfumo wa Usambazaji maji ambapo kazi zinazofanyika chini ya mradi huo ni pamoja na ujenzi wa matenki tisa (9) ya kuhifadhi na kusambaza maji  yenye ukubwa wa kuhifadhi lita milioni 3.0 hadi milioni 6.0, lakini pia ujenzi wa vituo vine(4) vya kusukuma maji, ununuzi na ufungaji wa pampu kubwa 16 za kusukuma maji, ununuzi wa transfoma  na ufungaji njia za umeme wa msongo mkubwa, ununuzi na ulazaji wa mabomba makubwa ya ugawaji maji na ulazaji wa mabomba ya usambazaji maji yatakayokuwa na urefu wa kilomita 477.
Mradi huu utanufaisha maeneo ya Salasala, Bunju, Wazo, Makongo, Changanyikeni , Bagamoyo, Mpiji, Zinga, Kiromo,Kitopeni, Ukuni, Kerege, Buma, Mataya na ukanda maalum wa EPZA ambayo ni maeneo yanayohudumiwa na mtambo wa maji wa Ruvu Chini.
Aidha maeneo mengine yatakayonufaika na mradi huu ni yale yaliyopo kati ya Mbezi Louis, Kiluvya, Kibamba,Mbezi, Makuzi, Makabe, Malamba mawili na Msigani. Maeneo yote haya hupata huduma kutoka Mtambo wa Ruvu Juu ambao ulizinduliwa na Mhe. Rais wa Jamhurim ya Muungani wa Tanzania Juni 21, 2017.
 Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Isack Kamwele, akiteremka kutoka juu ya tenki la maji linalojengwa huko Mabwepande nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam, leo Desemba 5, 2017, wakati wa ziara yake ya siku mbili kukagua miradi ya maji inayoendeshwa na DAWASA

 Mhandisi Kamwele, mtendaji Mkuu wa DAWASA, Mhandisi Romanus Mwang'ingo wakimsikiliza Mkandarasi, wapili kulia), na Mtendaji Mkuu wa DAWASCO, Mhandisi Cyprian Luhemeja wakitembelea eneo la ujenzi wa trenki la kuhifandia maji, Mabwepande nje kidogo ya jijji


 Mhe. Waziri Mhandisi Kamwele, (wapili kushoto), Mtendaji Mkuu wa DAWASA, Mhandisi Romanus Mwang'ingo wakimsikiliza Mkandarasi,   Mhandisi P.G. Rajani wa kampuni ya WAPCOS limited ya India.

 Mhe. Waziri Kamwele, (kushoto), akifafanua jambo, wakati akipatiwa maelezo na Mkandarasi kutoka kampunin ya India ya WAPCOS, Mhandisi P.G. Rajani

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...