Mwili wa Mpendwa wetu mpiganaji  unatarajia kuzikwa leo Januari 5, 2018 baada ya Swala ya Ijumaa na Maziko yatafanyika katika Makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam.
Msiba upo nyumbani kwa Marehemu Sinza Madukani  Mtaa wa Weruweru (Njia ya Namnani Hotel) Nyumba na 26. 

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa, shughuli zote ikiwa ni pamoja na za kuswalia maiti zitafanyika nyumbani kwa marehemu kabla ya kupelekwa makaburini Kisutu.
Marehemu Athumani Hamisi, aliyekuwa mpiga picha mkuu wa HabariLeo,  alifariki jana asubuhi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alikofikishwa kwa matibabu baada ya kuzidiwa ghafla usiku akiwa nyumbani kwake.
TUNATOA POLE KWA WOTE MLIOFIKWA NA MSIBA HUU.
 Baadhi ya waombolezaji wakiwa nyumbani kwa aliyekuwa mpigapicha wa magazeti Habari Leo, marehemu Athumani Hamisi nyumbani kwake Sinza jijini.
 Baadhi ya ndugu wakiwa msibani.
Waombolezaji.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...