NA TIGANYA VINCENT
SERIKALI ya Mkoa wa Tabora imetaka
watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge ambao wamechoshwa na ufanyaji kazi
kwa kuzingatia kasi ya Awamu ya Tano ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania wametakiwa kuandika barua za kuacha kazi ili kuwapisha ambao wataweza kuendana na
kasi hiyo.
Kauli hiyo ilitolewa jana wilayani
Sikonge na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri wakati akizungumza na watumishi
wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge kufuatia baadhi yao kutoroka zoezi la
upandaji miti na wengine kushindwa kutekeleza majukumu yao katika zoezi hilo.
Alisema kuwa wapo watu wengi ambao
wanahitaji kufanyakazi lakini hawana fursa hiyo, kama mtu anaona kazi
zinazotolewa na viongozi ni bughuza kwake ni vema akajiondoa kwa hiari yake
kabla hajachukuliwa hatu ikiwemo kuondolewa.
Mwanri alisema kuwa haiwezekani
mtumishi wa umma akachagua kazi za kufanya na kutofanya kwa kuwa kufanya hivyo
ni kinyume cha maelekezo ya barua yake ya ajira.
“Mlipopata barua zenu za ajira
zilikuwa zinaeleza kuwa zinaorosha kazi ambazo mtafanya na kumalizia kuwa na
kazi nyingine ambazo utapangiwa na viongozi wao, na kazi hizo ni pamoja na
kupanda miti” alisema Mwanri.
Alisema kuwa haiwezekani Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anaagiza kila Mkoa na kila Wilaya na
kila kijiji kipande miti kisha wanatokea watumishi wanakaidi kwa kudai kuwa sio
sehemu ya majukumu.
Mwanri alisema kuwa kama Mtumishi
wa Umma anaona kuwa upandaji miti kwake sio jukumu lake ni vema akaandika barua
na akaondoka kwa amani ili aende kwa mwajiri mwingine anayeona anamfaa.
Alisema kuwa suala la kupanda miti
ni kila mkazi wa Tabora wakiwemo watumishi wa umma na wananchi.
Mwanri alisema kuwa miti si mali ya
Mkuu wa Mkoa , wala Mkuu wa Wilaya bali ni kwa ajili ya faida ya wakazi wote wa
Tabora.
Alisema kuwa kukitokea jangwa
hakutamuathiri Mkuu wa Mkoa au viongozi pekee hata wale wanaojifanya hawataki
kupanda miti.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...