Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Kapteni (mstaafu) Mhe. George Mkuchika (Mb) ameiomba Serikali ya India kuendelea kuwajengea uwezo watumishi wa umma nchini.

Mhe. Mkuchika amesema hayo leo katika kikao na Balozi wa India nchini Mhe. Sandeep Arya ambaye ameahidi nchi yake kuendelea kutoa ufadhili katika fani mbalimbali kwa Watanzania.

“Watumishi kujengewa uwezo katika maeneo yanayohusu TEHAMA, Afya na Viwanda yatasaidia sana nchi yetu” Mhe. Mkuchika amesema mpango wa maendeleo wa Taifa wa 2025 unatilia mkazo viwanda ili kuleta mabadiliko ya uchumi na jamii.

Balozi Sandeep Arya kwa upande wake amesema nchi yake imepanga kwa siku za usoni kuendesha warsha na mafunzo kwa njia ya kieletroniki (e-corses) ambapo katika eneo la Afya amesema ili kujenga uwezo zaidi utafanyika utaratibu wa kubadilishana wataalam wa afya kati ya nchi yake na Tanzania.

“Tunapanga pia kuleta watalaam na kutoa mafunzo hapa Tanzania” Balozi Arya amesema na kuongeza kwa mwaka huu 2018 wameongeza mafunzo kuhusu vita dhidi ya madawa ya kulevya ikiwamo matumizi na usafirishaji wake.

Imetolewa na
Florence Lawrence
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano-UTUMISHI
05.01.2018
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Kapteni (mstaafu) Mhe. George Mkuchika (Mb), katikati, akiwa katika kikao na balozi wa India nchini Mhe.Sandeep Arya, wa pili kutoka kushoto.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Kapteni (mstaafu) Mhe. George Mkuchika (Mb), akiwa katika kikao na balozi wa India nchini Mhe.Sandeep Arya, wa pili kutoka kushoto

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...