*Rais Dkt.Magufuli apiga marufuku, asema asisikie mchango wa aina yoyote shuleni

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

Hivyo ndivyo unavyoweza kuelezea baada ya Rais Dkt.John Magufuli kusema ni marufuku watoto walioko shuleni kuchangishwa mchango wa aina yoyote na akisikia kuna shule katika wilaya fulani ambayo watoto wanafukuzwa kwa kutochangia basi huyo Mkurugenzi ajihesabu hana kazi.

Ametoa kauli hiyo leo Ikulu jijini Dar es Salaam baada ya kukutana na Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi) Sulemani Jaffo na Waziri wa Elimu ,Sayansi,Teknolojia na Ufundi Profesa Joyce Ndalichako ambapo ameagiza mawaziri hao ambao wanahusika na elimu kusimamia hilo na ni kuanzia leo.

"Kwa taarifa hii mkawaeleze wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya na wakurugenzi nikisikia kuna shule katika wilaya fulani ambapo watoto wanarudishwa kwa sababu ya kukosa michango, Mkurugenzi wa wilaya hiyo ajue hana kazi.Na haya maagizo yanaanza leo.Nimemueleza Waziri na Waziri mwenzake kusimamia hili,maofisa elimu wote nao wasimamie hili kwani wanalipwa kwa ajili hiyo,"amesema.

Rais,Dk.Magufuli amesema haiwezekani kutoa elimu bure halafu kero zikawa zinaongezeka na anatambua idadi ya wanafunzi imeongezeka lakini hiyo changamoto inatakiwa kubebwa na Serikali na kwamba hicho kisiwe kisingizio."Haiwezani tutoe elimu bure halafu kero zinaongezeka,"amesema.

Amesema sasa hivi watoto wanaacha kwenda shule kwa sababu michango inayotolewa tolewa, hivyo mawaziri hao wasimamie hilo na asisikie watoto wanarudishwa kwa sababu ya michango.

Dkt.Magufuli amesema hataki kusikia mahali popote wananchi wanalalamikia michango huku akitumia nafasi hiyo kuwawaambia walimu ni marufuku kushika mchango wowote.

"Ni marufuku mwanafunzi kurudishwa kwasababu ya kukosa mchango wa maabara,ni marufuku mwanafunzi kurudishwa kwasababu ya mchango wa madawati.Ni marufuku kuchangisha mchango wowote.Kama kuna anayetaka kuchangia iwe kwa hiyari yake anapeleke kwa Mkurugenzi.

"Nikisikia wanafunzi wanachangishwa kwasababu ya michango kuanzia mkuu wa mkoa , mku wa wilaya na mkureugenzi wa eneo husika wote wataondoka,"amesema Rais Dkt.John Magufuli

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...