Na Said  Mwishehe, Blogu ya jamii
MBUNGE wa  Chalinze mkoani Pwani, Ridhiwani Kikwete amemuonesha Naibu wa  Waziri wa  Nishati, Subira Mgalau maeneo yenye mahitaji maalumu ya kupatiwa nishati ya umeme. 

Akizungumza na wananchi wa  Kata ya Talawanda akiwa ameongozana na Waziri wa  Nishati, Subira Mgalau, Ridhiwani ametumia nafasi hiyo kuomba umeme na hasa  katika  hospitali kwa lengo la kufanikisha upatikanaji wa huduma za afya hasa kwa akina mama wajazito na watoto. 

Pia amemsisitiza umeme uwekwe kwenye shule ili kuwapa nafasi wanafunzi wa Kata ya Talawanda na Chalinze kwa ujumla kujisomea wakati wowote. 

"Mheshimiwa Naibu Waziri wa Nishati,  moja ya changamoto iliyopo jimboni kwetu na hapa katika Kata ya Talawanda ni zahanati yetu kutokuwa na umeme, hivyo tunaomba mtusaidie na pia katika shule.
 Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu na mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete wakiwasalimia wananchi wa kata ya Talawanda.
 Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete(kushoto) akizungumza jambo na Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu walipokuwa Kata ya Talawanda jimboni Chalinze kwa lengo la kuzungumza na wananchi.
Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalau(wa pili kulia) akizungumza na mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete wakiwa katika Kata ya Talawanda.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...