. Watanzania wametakiwa kuenzi sanaa na utamaduni waliona kwa ajili ya kizazi kijacho ili kukijendea uzalendo wa kupenda nchi yao. 

Hayo yamesema Mkurugenzi wa Tamasha la Sauti za Busara, Yusuf Mahmoud wakati akielezea ujio wa Tamasha la 15 linalotarajiwa kufanyika Ngome Kongwe, Unguja - Zanzibar kwa kushirikisha wanamuziki na vikundi mbali mbali vya sanaa kutoka pande zote za bara la Afrika na Ulaya.

 “Katika Tamasha hili, ni sehemu ambapo watu wenye weledi wa sanaa mbalimbali hukutana, kuanzia kwa wakurugenzi wa matamasha mpaka kwa wazalishaji wa muziki, mameneja wa wanamuziki, wasambazaji wa muziki, wote hawa huja hapa Zanzibar mwezi Februari kuja kushuhudia utamu wa midundo ya muziki wa Ukanda wa Afrika Mashariki,” anasema Mkurugenzi wa Tamasha la Sauti za Busara, Yusuf Mahmoud.

Anaongeza kuwa, “Hili siyo tu tukio ambalo watumbuizaji wa Tamasha pekee huhudhuria, bali hata baadhi ya wanamuziki ambao hawapo katika orodha ya kutumbuiza huja kwa minajili ya kujifunza kutoka kwa wale wanaofanya maonesho mbalimbali, na pia hupata fursa ya kufahamiana na wadau muhimu wa tasnia yao na kutengeneza mahusiano ya kikazi kwa miezi ijayo, hata zaidi ya hapo baada ya tamasha kuisha.” Likisifika kuwa miongoni mwa matamasha yanayoheshimika, Sauti za Busara likiwa na kauli mbiu ya “Kuunganishwa na Muziki” kwa mwaka huu, linawakutanisha pamoja zaidi ya wanamuziki 460 katika visiwa vya Zanzibar.

Likiwa ni tamasha ambalo limeshuhudia ukuaji mkubwa katika uadhimishwaji wake na mwaka huu ukiwa wa 15, Tamasha hili linavutia wataalamu wa habari na muziki kutoka katika kila pembe ya Afrika, Ulaya na mahali pengine, ambapo hutoa jukwaa la kipekee kwa wanamuziki wa Afrika Mashariki kuutanganza muziki wao duniani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...