Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 31 Januari, 2018 amezindua mfumo wa uhamiaji mtandao (e-Immigration) ambao utasaidia kuimarisha ulinzi na usalama wa mipaka ya nchi, kudhibiti ukusanyaji wa maduhuli ya Serikali na kuimarisha utoaji wa huduma za kiuhamiaji kwa raia wa Tanzania na wageni wanaoingia na kuishi hapa nchini kwa madhumuni mbalimbali.
Kabla ya kuzindua mfumo wa uhamiaji mtandao Mhe. Rais Magufuli amekagua teknolojia iliyotumika katika mfumo huo ikiwa ni pamoja na kuchukuliwa alama za vidole na baadaye kupatiwa pasipoti mpya ya kielektronikia (e-Passport) ambayo pia imeanza kutolewa leo.
Pasipoti mpya za kielektronikia pia zimetolewa kwa viongozi wengine wakuu wa Serikali, Bunge na Mahakama wa Tanzania Bara na Zanzibar, waliohudhuria uzinduzi huo.


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli  akiweka sahihi kwa ajili ya kujipatia pasipoti yake mpya  makao makuu ya Idara ya Uhamiaji Kurasini jijini Dar es salaam leo Januari 31, 2018.  

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt  John Pombe Magufuli  akiwa na  Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein akisubiri hatua inayofuata  baada ya kuweka sahihi kwa ajili ya kujipatia pasipoti yake mpya ya kielektronikia makao makuu ya Idara ya Uhamiaji Kurasini jijini Dar es salaam leo Januari 31, 2018. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akionesha kwa furaha passipoti yake mpya  ya kielektronikia baada ya kuipokea kutoka kwa Waziri wa mambo ya Ndani Dkt. Mwigulu Nchemba makao makuu ya Idara ya Uhamiaji Kurasini jijini Dar es salaam  Januari 31, 2018.



 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akionesha kwa furaha passipoti yake mpya  ya kielektronikia baada ya kuipokea kutoka kwa Waziri wa mambo ya Ndani Dkt. Mwigulu Nchemba makao makuu ya Idara ya Uhamiaji Kurasini jijini Dar es salaam Januari 31, 2018. Kushoto ni Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein na kushoto kwa Waziri ni Kamishna Mkuu wa Uhamiaji Dkt. Peter Makakala.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt  John Pombe Magufuli   akionesha kwa furaha passipoti yake mpya  ya kielektronikia baada ya kuipokea kutoka kwa Waziri wa mambo ya Ndani Dkt. Mwigulu Nchemba makao makuu ya Idara ya Uhamiaji Kurasini jijini Dar es salaam Januari 31, 2018. 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt  John Pombe Magufuli  akiiangalia  kwa furaha passipoti yake mpya  ya kielektronikia baada ya kuipokea kutoka kwa Waziri wa mambo ya Ndani Dkt. Mwigulu Nchemba makao makuu ya Idara ya Uhamiaji Kurasini jijini Dar es salaam  Januari 31, 2018. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt  John Pombe Magufuli  akipokea passipoti yake mpya  ya kielektronikia  kutoka kwa Waziri wa mambo ya Ndani Dkt. Mwigulu Nchemba makao makuu ya Idara ya Uhamiaji Kurasini jijini Dar es salaam  Januari 31, 2018. 
 Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein  akipokea pasipoti yake mpya ya kielektronikia kutoka kwa Waziri wa mambo ya Ndani Dkt. Mwigulu Nchemba makao makuu ya Idara ya Uhamiaji Kurasini jijini Dar es salaam  Januari 31, 2018.  
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan  akionesha kwa furaha passipoti yake mpya  ya kielektronikia baada ya kuipokea kutoka kwa Waziri wa mambo ya Ndani Dkt. Mwigulu Nchemba makao makuu ya Idara ya Uhamiaji Kurasini jijini Dar es salaam  Januari 31, 2018  PICHA NA IKULU

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...