Na Agness Francis Globu ya jamii 

 MABINGWA wa Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, wanaendelea vizuri kufanya mazoezi kuelekea mchezo ujao wa hatua ya 16 bora ya michuano ya Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) dhidi ya KMC iliyopanda daraja. 

 Katika msimu huu kikosi hicho kimefanikiwa kufika tena hatua ya 16 bora ambapo watashuka katika dimba la Uwanja wa Azam Complex wakiwa wageni dhidi ya timu hiyo siku ya kesho saa moja usiku. Ambapo kikosi hicho kina historia ya kufika mara mbili hatua ya 16 bora ya Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) kwa misimu miwili iliyopita tangu michuano hiyo iliporudishwa tena mwaka 2015. 

 Msimu wa 2015/2016 wakati kikosi hicho kikifika hatua ya fainali na kufungwa na Yanga mabao 3-1, Azam FC ilikutana na Panone ya mjini Moshi kwenye hatua ya 16 bora katika mechi ngumu iliyofanyika Uwanja wa Ushirika, ambapo matajiri hao walitoka nyuma kwa bao moja na kushinda 2-1, mabao yaliyofungwa na wachezaji wa zamani wa timu hiyo, beki Pascal Wawa na mshambuliaji Allan Wanga. 

 Azam FC iliyoishia hatua ya nusu fainali msimu uliopita baada ya kufungwa na Simba bao 1-0, ilifuzu hatua ya robo fainali baada ya kuitoa Mtibwa Sugar kwa kuipa kipigo cha 1-0, kwenye hatua ya 16 bora mchezo ulipofanyika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam, bao likifungwa na winga Ramadhan Singano 'Messi'.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...