Naibu waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi mhe. Angelina Mabula ameshangazwa na uwepo wa majalada ya ardhi katika halmashauri za Butiama na Musoma ambayo wamiliki wake hawafahamiki na majalada hayo kujulikana kama ‘’ndugu mhusika’’.

Akiwa katika ziara yake ya siku tatu ya kushughulikia migogoro ya ardhi pamoja na kukagua mfumo wa ulipaji kodi ya ardhi mkoani Mara mhe. Mabula alisema majalada hayo yamekuwa na matatizo ya viwango vya kulipa kodi kwa kuwa yanaonekana kuwa deni huku mmiliki akitaka kumilikishwa upya kwa gharama ndogo.

Kufuatia mkanganyiko huo, naibu waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi aliyakabidhi majalada yenye utata kwa taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) kwa uchunguzi zaidi ili kubaini kama suala hilo limefanyika kimakosa ama ni kwa makusudi.‘’Mtu anamilikishwa leo kwa pesa ndogo sana halafu za huko nyuma zinapotea hapa kuna mchezo unafanyika kupunguza mapato ya serikali’’ alisema Mabula.
Naibu waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Angelina mabula akizungumza na watumishi wa halmashauri za Mji na Wilaya ya musoma mkoa wa Mara.
Baadhi ya watumishi wa kanda wa Wizara ya Ardhi nyumba na maendeleo ya Makazi wakimsikiliza Naibu waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Angelina mabula wakati wa ziara yake mkoani Mara.
Mkuu wa Wilaya ya Musoma Dk. Vicent Anney Naano akizungumza wakati wa ziara ya naibu waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi mkoani mara.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...