Na John Nditi, Kilombero.

HALMASHAURI ya wilaya ya Kilombero , mkoani Morogoro wamewakatia  kadi za   Mfuko wa Afya ya Jamii  (CHF ) iliyoboreshwa  wazee wasiojiweza zaidi ya 7,800 waliopo katika  kata  26  ili kuwawezesha kupata  huduma bora za matibabu katika vituo vya  Afya, Zahanati na hospitali na wategemezi wao.

Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri  hiyo , Dennis Londo   alisema hayo  mbele ya  Katibu tawala mkoa wa Morogoro, Clifford Tandari, kabla ya zoezi la ugawaji  kadi za CHF Iliyoboreshwa  kwa baadhi ya wazee wapatao  2,100 kutoka  vijiji 23 vya kata saba za Tarafa ya Mlimba.

Londo  alisema   kuwa , hadi sasa  kiasi cha Sh milioni 13.3 zimetumika  kwa ajili ya mpango wa kuwakatia wazee wasiojiweza  bima  ya  afya ya CHF Iliyoboreshwa.Hata hivyo alisema , halmashauri hiyo imejipanga  kuhakikisha wazee wanapatiwa bima ya Afya CHF iliyoboreshwa na lengo  ni  kuwafikia  wazee wasiojiweza  zaidi ya  15,000  katika kata zote 26.

“ Halmashauri ya wilaya hii imejipanga vyema na inatekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM  na miongoni mwa mam ohayo ni kundi la wazee wasiojiweza wamenufaka na huduma ya bima  ya afya” alisema Londo.
 Katibu Tawala wa mkoa wa Morogoro, Clifford Tandari  ( wapili  kushoto) akimkabidhi kadi ya bima ya afya ya Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) Iliyoboreshwa mzee  Petro Karubandika mkazi wa kata ya Mlimba , halmashauri ya wilaya ya Kilombero  wakati wa zoezi la ugawaji  kadi  hizo kwa wapatao  2,100 kutoka  vijiji 23 vya kata saba za Tarafa ya Mlimba na (  kushoto) ni  mkuu wa wilaya ya Kilombero, James Ihunyo na ( watatu kushoto) ni Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Kilombero, Dennis Londo.
 Katibu Tawala wa mkoa wa Morogoro, Clifford Tandari  ( wapili kushoto) akimkabidhi kadi ya bima ya afya ya Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) Iliyoboreshwa   Nelasi Nyingi , mkazi wa kata ya Mlimba , halmashauri ya wilaya ya Kilombero  wakati wa zoezi la ugawaji  kadi  hizo kwa wapatao  2,100 kutoka  vijiji 23 vya kata saba za Tarafa ya Mlimba (  kushoto ) ni mkuu wa wilaya ya Kilombero, James Ihunyo na ( watatu kushoto) ni Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Kilombero, Dennis Londo.
 Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri   ya Kilombero , Dennis Londo  ( kulia) akitoa maelezo mafupi ya mapango wa kuwakatia bima ya afya wazee  wasiojiweza kwa  Katibu tawala mkoa wa Morogoro, Clifford Tandari ( wapili kutoka kushoto) wakati wa  zoezi la ugawaji  kadi za CHF Iliyoboreshwa  kwa  wazee wapatao  2,100 wa  vijiji 23 vya kata saba za Tarafa ya Mlimba.
Baadhi ya wazee wa kata saba za tarafa ya Malimba , halmashauri ya wilaya ya Kilombero wakimsikiliza mgeni rasmi Katibu tawala mkoa wa Morogoro, Clifford Tandari  ( hayupo pichani) wakati wa  zoezi la ugawaji  kadi za CHF Iliyoboreshwa  kwa  wazee wapatao  2,100 wa  vijiji 23 vya kata saba za Tarafa ya Mlimba.  ( Picha na John Nditi).

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...