Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii
MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Latifa Mussa a.k.a Miss KK Jumamosi ya Februari 25, mwaka huu anatarajia kuzindua video yake ya kwanza inayokwenda kwa jina la "Wananuna".
Uzinduzi wa video hiyo yenye Mandhari ya tofauti tofauti utafanyika katika kiota cha Pallet Mbezi Beach jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na wasanii mbalimbali wakiwemo wa kutoka Wanene entertainment ambao ni moja kati ya wafadhili wa msanii KK.
Katika Video ya Wananuna ambayo inamandhali ya kuvutia hasa ikiwa imeshutiwa jijini Arusha na Dar es Salaam na kufanyiwa editing nchini Afrika Kusini, wananchi watapa fursa ya kuona hata utalii wa ndani.

Msanii KK  aliyekuwa akifanya shughuli zake za mziki nchini Afrika Kusini kwa muda mrefu amesema, lengo lake kubwa na kufanya muziki nchini ni kuwafanya wanamuziki kutoka Tanzania wana perfoam Afrika Kusini na vilevile kwa Afrika Kusini.
Aidha katika usiku huo kutakuwa na usiku wa Black Carpet. " Napenda kuwaambia wasanii wapya wanaochipukia kwenye muziki, watuliee, waache papara kuwa na malengo na wasikubali kuyumbishwa."
 Sherehe za uzinduzi huo zinatatajiwa kuanza SAA Moja usiku na watu wakwanza kufika kuanzia muda huo mpaka saa tatu watapata kuponi za vinywaji za bure na kati yao watapata vocha kutoka kwa mdhamini wake Coast airline kwenda mbuga za wanyama za Ruaha kwa Siku  mbili.
Msanii wa Muziki, Latifa Mussa, mwenye shati nyekundu, akizungumza na waandishi wa Habari juu ya uzindizi wa video yake inayokwenda kwa jina la wanune inayotarajiwa kuzinduliwa February 24, katika kiota cha Pallet Mbezi beach, pembeni ni Meneja wake, Erikson Kinywele aka DJ Kinywele

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Itakuwa nzuri sana, Tumekuwa tukifuatilia mziki wake pia kumsapoti hivo naamini hata sisi BongoSwaggz tutaipaisha ikitoka.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...