Na Mathias Canal, Songwe
Naibu
Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko leo 22 Februari 2018 ameanza
ziara ya kikazi katika Mkoa wa Songwe ambapo pamoja na mambo mengine
atatembelea na kukagua eneo la mgodi tarajiwa wa Bafex linalotarajiwa
kuanza uchimbaji wa Madini ya dhahabu.
Maeneo
mengine atakayotembelea ni pamoja na mgodi wa uchimbaji dhahabu wa
Shanta Gold Mine uliopo katika kata ya Saza, Wilayani Songwe ambapo
atazungumza pia na wafanyakazi wa mgodi huo.
Sambamba
na hayo pia Naibu Waziri wa Madini atazungumza na wachimbaji wadogo
kwenye mkutano ulioandaliwa Mara baada ya kutembelea maeneo ya
uchimbaji.
Mara
baada ya kuwasili katika Mkoa wa Songwe Mhe Biteko amesifu juhudi za
mbunge wa Jimbo la Songwe Mhe Philiph Mulugo kutokana na uwajibikaji
mkubwa katika kuwasemea wananchi wa jimbo hilo hususani katika
kuimarisha uchumi wa wananchi kupitia sekta ya Madini.
Naibu Waziri wa Madini, Mhe Doto Mashaka Biteko akizungumza mara baada ya kupokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Songwe kwa ajili ya ziara ya siku mbili ya kikazi katika mkoa wa Songwe, Leo 22 Februari 2018.
Naibu Waziri wa Madini, Mhe Doto Mashaka Biteko akisisitiza jambo mbele ya Kamati ya ulinzi na usalama Wilaya ya Songwe, na Kamati ya siasa ya CCM Wilaya hiyo mara baada ya kuwasili Mkoani Songwe kwa ziara ya kikazi, Leo 22 Februari 2018.
Mkuu wa wilaya ya Songwe, Mhe Samwel Jeremiah akieleza changamoto za wachimbaji wadogo katika Wilaya hiyo mbele ya Naibu Waziri wa Madini, Mhe Doto Mashaka Biteko wakati akisoma taarifa ya Mkoa wa Songwe kwa niaba ya mkuu wa Mkoa huo, Mhe Chiku Galawa, Leo 22 Februari 2018.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...