Na Lydia Churi-Mahakama ya Tanzania
Viongozi wanaohusika na Oparesheni za kuzuia uhalifu wameshauriwa kufuata na kuzingatia sheria inayoongoza namna ya ukusanyaji wa ushahidi ili kuepuka kuharibu ushahidi kabla haujawasilishwa Mahakamani na kupelekea kesi nyingi kuharibika kwa kukosa ushahidi au Mahakama kushindwa kutoa hukumu zinazoendana na kosa husika.
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma ameyasema hayo wakati akizungumza na viongozi wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Uyui alipomtembelea Mkuu wa wilaya hiyo ikiwa ni sehemu ya ziara yake inayoendelea Mahakama Kuu kanda ya Tabora. 
 Akitolea mfano wa Oparesheni za uteketezaji wa dawa za kulevya yakiwemo mashamba ya bangi, Jaji Mkuu amesema ushahidi kuteketezwa bila ya kufuata utaratibu huathiri mienendo ya kesi Mahakamani.
Akizungumzia suala la Maadili ndani ya Mahakama, Jaji Mkuu amewaomba Wakuu wa mikoa pamoja na Wakuu wa wilaya ambao anawatambua kama walezi wa Mahakama kushirikiana kwa karibu zaidi na Mahakama ili kuhakikisha wanawahudumia wananchi ipasavyo katika suala zima la utoaji wa Haki.
 Kuhusu kusogeza huduma za kimahakama karibu Zaidi na wananchi, Jaji Mkuu amesema Mahakama kwa kushirikiana na Benki ya Dunia inao Mpango wa kuanzisha Mahakama zinazotembea (Mobile Courts) ili kuwafikia wananchi walio mbali na huduma za kimahakama hasa katika wilaya ya Uyui mkoani Tabora 
 Naye Mkuu wa wilaya ya Tabora na Kaimu Mkuu wa wilaya ya Uyui, Queen Mlozi   alimweleza Jaji Mkuu kuwa kwa namna wilaya ya Uyui ilivyokaa kijiografia, wananchi hulazimika kufuata huduma za kimahakama umbali wa Zaidi ya kilometa 150 katoka Loya kwenda Kigwa mkoani Tabora.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...