Na Ismail Ngayonga.

SERIKALI ya Jamhuri ya Poland mapema mwezi April mwaka huu inatarajia kufungua upya Ofisi za Ubalozi wa nchi hiyo hapa nchini ambazo zilifungwa kwa muda, hatua inalenga kuimarisha uhusiano na ushirikiano baina ya Mataifa hayo.

Hayo yamesemwa leo Ijumaa (Februari 23, 2018) Jijini Dar es Salaam na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe wakati alipokuwa Salamu za Rais wa Poland kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli.

Dkt. Mwakyembe alisema hatua zote muhimu za ufunguzi wa Ubalozi huo, taratibu zote muhimu kwa ajili ya ufunguzi Ofisi za Ubalozi huo tayari zimekamilika na kuongeza kuwa kufunguliwa kwa ubalozi kutazidi kudumisha ushirikiano na urafiki wa muda mrefu baina ya Tanzania na Poland pamoja na kuimarisha diplomasia ya uchumi baina ya mataifa hayo.

 “Serikali ya Jamhuri ya Poland imekuwa na ushirikiano wa muda mrefu na Tanzania, ambapo matunda ya ushirikiano ni kwa Serikali yetu kupata wa mkopo wa masharti nafuu uliofanikisha uanzishaji wa kiwanda kikubwa cha matrekta kibaha Mkoani Pwani” alisema Dkt. Mwakyekmbe.
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Harrison Mwakyembe (kushoto) akisalimiana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais wa Poland Mhe. Krzysztof Szczerski  wakati alipoleta salamu za Rais wa Poland na mwaliko kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Magufuli, mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Harrison Mwakyembe (kulia) akipokea salamu za Rais wa Poland na mwaliko kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Magufuli toka kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais wa Poland Mh.Krzysztof Szczerski.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais wa Poland Mh.Krzysztof Szczerski (kushoto) akiteta jambo na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Harrison Mwakyembe mara baada ya kukabidhi  salamu za Rais wa Poland na mwaliko kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Magufuli mapema hii leo jijini Dar es Salaam.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...