Na Said Mwishehe,Globu ya Jamii

JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linamshikilia, Rajabu Mohamed(25) anayejifanya ni Freemason na amekuwa akifanya ukatili,unyanyasaji wa kijinsia na kupora mali hasa kwa wanawake.

Pia amekuwa akiwatishia wanawake anaowafanyia ukatili kuwa wakitoa taarifa zake atawaua kwa kuwanyonya damu na kuwakata sehemu zao za siri.

 Akizungumza leokukamatwa kwa mtu huyo, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema Februari 25 mwaka huu Polisi walimkata akiwa maeneo ya Mwenge  ambako ndiko anakoishi.

Amesema mtu huyo amekuwa akitumia gari naomba T 172 BLH aina ya Fun Cargo rangi ya Silva ambapo amekuwa akikamata wanawake kwa kuwalaghai kuwa ni mfanyabiashara na wakishaingia kwenye gari lake hutumia nguvu na kuwanyang'anya vitu vilivyomo kwenye mabegi.

Amesema baada ya kunyang'anya mabegi hayo huanza kuwazungusha barabarani huku akiwatisha kuwa yeye ni  Freenason na kuwa atawaua kwa kuwanyonya damu au kukata sehemu zao za siri.

"Kupitia vitisho hivyo huwalazimu wotoe namba za siri za simu zao na kuchukua kadi zao za benki na kuwaibia fedha zao kwenye ATM na baada ya hapo kuwashusha na kuwatelekeza kwenye vichochoro.

"Huyu mtu tumemuhoji anasema kwa sasa ameacha,ukimuangalia sura yake ni ya binadamu lakini ni mnyama wa hali ya juu kabisa.Amefanya mambo mengi ya kishenzi.

" Tunaendelea na taratibu nyingine na baada ya hapo atapelekwa mahakamani ili ajibu tuhuma za makosa ambayo yanamkabili ,Sheria tunataka ichukue mkondo wake,"amesema Kamanda Mambosasa.

Ameongeza kuwa matukio ambayo anatuhumiwa kufanya mtu huyo kwa baadhi yawanawake ambao wametoa taarifa zake hata mnyama ambaye yupo mbugni na  wanyama wezake  hawezi kufanya.

Amesema kuwa iwapo atakuwa na Ukwimwi maana yake atakuwa ameambukiza wanawake wengi na hafai kabisa kwenye jamii.

Mambosasa ametoa rai kwa watu ambao wamefanyiwa ukatili na mtuhumiwa huyo kufika polisi kutoa taarifa."Si mtu mwema hata kidogo ingawa sura yake ni ya kibinadamu,"

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...