Usajili wa mbio za Kilimanjaro Premium Lager Marathon zinazotarajiwa kufanyika jumapili ijayo mjini Moshi umekuwa mkubwa huku wakazi wa Dar es Salaam na mikoa ya jirani wakimiminika kukamilisha zoezi hilo na kupokea namba zao za ushiriki.

Zoezi hilo limefanyika kwa ukamilifu Jumamosi na Jumapili katika Viwanja vya Mlimani City ambao walidhamini eneo hilo la kujisajili kama njia ya kuunga mkono juhudi za kukuza na kuendeleza michezo hususan riadha.

“Tumeridhishwa sana na muitikio wa watanzania na kwa kweli mwaka huu muamko ni mkubwa zaidi kwani mbio hizi zimezidi kuwa maarufu na kubwa mwaka hadi mwaka,” allisema Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, Pamela Kikuli ambaye bia yake ndio mdhamini mkuu wa mbio hizi.

Alisema wana uhakika washiriki watazidi 10,000, idadi ambayo ilifikiwa mwaka jana. “Mwaka huu sisi kama Kilimanjaro Premium Lager tunawakumbusha wateja wetu kuwa twende Moshi kushiriki, tufurahie bia yetu namab moja baada ya kukimbia lakini pia tukumbuke kutoendesha vyombo vya moto huku tukiwa tumetumia kilevi,” alisema Meneja huyo.

Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael alisema wao kama wadhamini wa mbio za kilometa 21wameona muamko mkubwa na wanatarajia washiriki wengi zaidi katika mbio hizo za half marathon.

Mbio za mwaka huu, ambazo zinaandaliwa na Wild Frontiers na Dep Blue Media na kuratibiwa kitaifa na kampuni ya Executive Solutions, zitafanyika katika Chuo Kikuu Cha Ushirika Moshi (MoCU) Machi 4 kuanzia saa 12 asubuhi.
Wakazi wa Dar es Salaam wakijiandikisha kushiriki katika mbio za Kilimanjaro Premium Lager Marathon zitakazofanyika Mjini Moshi Machi 4, mwaka huu. Zoezi hilo lilifanyika katika viwanja vya Mlimani City.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...