Mkuu wa chuo cha usimamizi wa fedha "IFM"  Pro. Tadeo Satta akizungumza na wahitimu wa mafunzo ya Bima pamoja na wadau wa bima kwa nyanda za juu kusini katika hafla fupi ya mahafali ya wahitimu walio fanikiwa kumaliza mafunzo ya kuelewa na kutambuwa umuhimu wa Bima kwa mwezi Januari.HafLa hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa chuo kikuu huria jijini Mbeya ni moja ya muangaza kwa wananchi wa mkoa wa mbeya kukimbilia fursa hii kwa kupata mafunzo mafupi kisha kuhitimu na kukabidhiwa cheti chenye kukuwezesha kuwa wakala wa makampuni ya bima ikiwemo, "NIC -  Shirika la Bima laTaifa, ZIC - Shirika la Bima Zanzibar, Kampuni ya RELIANCE, JUBILEE, BRITAM, UAP, BUMACO, SANLAM, MGEN, ICE LION na IGT, kwa kujipatia kipato au Ajira.
Kutoka kushoto ni Meneja wa TIRA,Consolata Gabone akizungumza jambo katika hafla fupi ya kutunukiwa vyeti wahitimu wa mafunzo ya Bima yanayo tolewa na wakufunzi wa chuo cha usimamizi wa fedha "IFM'
Moja kati ya wanafunzi Pichani akipokea cheti mara baada ya kuhitimu mafunzo hayo ya kufahamu na kutambuwa umuhimu wa bima.
Baadhi ya wahitimu wakiwa wameketi katika hafla hiyo iliyofanyika jijini mbeya katika ukumbi wa Chuo kikuu Huria.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...