Na Victor Masangu, Chole Kisarawe .
WAKINAMAMA wajawazito katika kijiji cha Kihare kata ya Maluwi Wilaya ya Kisarawe, Mkoani Pwani waliokuwa wanakabiliwa na changamoto katika sekta ya afya kutokana na ukosefu wa kutokuwa na wodi maalumu ya kujifungulia kwa kwa kipindi cha muda mrefu na kuwalazimu kutembea umbari wa kilometa 15 kufuata huduma hatimaye kilio chao kimepata mkombozi baada kukamilika kwa jengo la wazazi.
Aisha Ramadhani na Fatma Iddy ni baadhi ya wakinamama ambao walisema kwa miaka mingi wamekuwa wanateseka pindi inapofika wakati wa kujifungua kutokana na zahanati ya Kihare ambayo walikuwa wanaitumia katika kupata huduma ya matibabu ilikuwa haina jengo la wodi ya wazazi hivyo ilikuwa inawalazimu kufunga safari ya umbari wa kilometa 15 kwa kutumia usafiri wa baiskeli,pikipiki au wakati mwingine kutembea kwa miguu.
Walisema kwamba hapo awali walikuwa wanapata shida kubwa wakati wa kujifungua kutokana na kutokuwepo kwa wodi ya kujifungulia hivyo walikuwa wanachanganywa na wagonjwa wengine wa kawaida kitu hali ambayo ji hatari kwa afya zao na mtoto, hivyo wameipongeza serikali ya awamu ya tano na juhudi za Mbunge wa jimbo lao kwa kuamua kujenga jengo hilo ambalo litakuwa ni msaada mkubwa katika utoaji wa huduma.
Waziri wa nchi ofisi ya Rais Tamisemi, Seleman Jafo akizungumza na baadi ya viongozi na watendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe, wakati wa ziara yake ya kikazi kwa ajili ya kukagua miradi mbali mbali ya maendeleo katika sekta ya afya, maji, barabara, pamoja na elimu pamoja na kuzungumza na wananchi.
Waziri wa nchi ofisi ya Rais Tamisemi, Seleman Jafo (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wauguzi na madaktari wa halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe, wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua miradi mbali mbai ya maendeleo pamoja na kuzungumz na wananchi.(PICHA ZOTE NA VICTOR MASANGU).
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...