KUANZISHWA kwa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi ni hatua muafaka katika mazingira ya sasa ambapo kuna ongezeko la maeneo ya uzalishaji hususan viwanda kunakokwenda sambamba na ongezeko la matukio ya athari zinazotokana na ajali, magonjwa ama vifo kutokana na kazi, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama amewaambia wabunge wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wakati wa warsha ya kujenga uelewa kwa wabunge kuhusu majukumu ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), mjini Dodoma Februari 3, 2018.

Mhe. Mhagama alisema warsha hiyo ni utekelezaji wa ombi lililotolewa na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria kutaka wabunge wajengewe uelewa wa shughuli za Mfuko huo. Akifafanua zaidi Mhe. Waziri alisema Mfuko uliundwa Julai 2015 chini ya kifungu cha 5 cha Sheria ya Fidia kwa wafanyakazi, sura 263 marejeo ya mwaka 2015 ili kulipa Fidia stahiki kwa mfanyakazi aliyeumia, kupata maradhi au kifo wakati akitekeleza majukumu yake ya kikazi kwa mujibu wa mkataba. 

Alisema, Serikali ilianzisha Mfuko huo kwa lengo la kuhakikisha kuwa wafanyakazi wanapata Mafao bora ya Fidia tofauti na Sheria ya zamani ya Fidia kwa Wafanyakazi ambayo viwango vyake vya Mafao ya Fidia vilikuwa vya chini mno. “Mathalan viwango vya juu vya Fidia kwa Mfanyakazi aliyepata ajali kazini ilikuwa ni shilingi 108,000/= huku Mfanyakazi aliyefariki katika ajali ama ugonjwa kutokana na kazi anayofanya kwa mujibu wa Mkataba wa ajira yake ilikuwa ni shilingi 83,000.” Alibainisha Mhe. Waziri.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama (MB), akizungumza kwenye warsha ya siku moja ya kuwajengea uelewa wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhusu majukumu ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), kwenye ukumbi wa Msekwa, Bungeni mjini Dodoma Februari 3, 2018. Kulia ni Mwenyekiti Mwenza wa Bunge, Mhe. Andrew Chenge, na katikati ni Mwenyekiti wa Warsha hiyo, ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Kamatui ya Bunge ya Katiba na Sheria na Mwenyekiti Mwenza wa Bunge, Mhe. Najma Giga.
Mhe. Najma Giga(katikati), akizungumza wakati wa ufunguzi wa warsha hiyo. Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria, iliishauri serikali juu ya umuhimu wa waheshimiwa wabunge kukutana nna wataalamu kutoka WCF ili kuwajengea uelewa wa shughuli za Mfuko. 
Mhe. Andrew Chenge, akizunhgumza kwenye warsha hiyo.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Bw. Masha Mshomba, akitoa mada juu ya uelewa wa jumla kuhusu utekelezaji wa Matakwa ya kifungu cha 5 cha Sheria ya Fidia kwa wafanyakazi, sura 263 marejeo ya mwaka 2015 mjini Dodoma leo Februari 3, 2018.
Baadhi ya waheshimiwa wabunge na viongozi wa WCF wakifuatilia warsha hiyo.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...