Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara (VPL) Yanga, kesho wanashuka dimbani kuvaana na kikosi cha Majimaji ya Songea " Wanalizombe" katika mchezo wa raundi ya 18 kwenye dimba la Uwanja wa Taifa.

Mechi hiyo itakayoanza majira ya saa 10 alasiri unatarajiwa kuwa wa ushindani kwa pande zote mbili,Yanga wakitaka kupata ushindi ili kuzidi kujiweka kwenye mazingira ya kutetea ubingwa wao huku Majimaji wakitaka kujinasua kutoka kwenye nafasi ya tatu kutoka chini.

Katika mchezo wa kwanza uliochezwa mkoani Songea kwenye Uwanja wa Majimaji Yanga walilazimishwa sare ya 1-1 wakisawazisha goli hilo kupitia kwa mshambuliaji wake wa kimataifa kutoka Zimbabwe Donald Ngoma.

Akizungumza na Globu ya jamii Mkuu wa Kitengo cha habari na Mawasiliano wa Yanga Dismas Ten amesema timu imeendelea  na mazoezi yake kama kawaida na kesho kitashuka dimbani kikiwakosa wachezaji watatu ambao hawajaanza kujumuika na wenzao kwenye mazoezi.

Amewataja wachezaji hao ni Amidi Tambwe, Donald Ngoma na Yohana Mkomola ambao wapo chini ya uangalizi wa daktar wakiuguza majeraha yao.

" Wachezaji watakaokosekana kwenye mchezo wa kesho dhidi ya Majimaji ni watatu ambao hawajaanza mazoezi na wenzao ni Donald Ngoma, Amisi Tambwe na Yohana Mkomola wakiwa chini ya uangalizi wa daktari," amesema Ten.

Yanga watashuka dimbani wakiwa na alama 34 wakishika nafasi ya pili nyuma ya vinara wa VPL Simba wakiwa kileleni kwa alama 38.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...