Na Leandra Gabriel, Globu ya jamii

RAIS mteule wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa ametangaza kuwa Uchaguzi Mkuu nchini humo unatarajiwa kufanyika Julai mwaka huu.

Tarehe ya uchaguzi huo itatangazwa hapo baadaye na hiyo ni baada ya utawala wa muda mrefu wa  takribani miaka 37 ya aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Robert Mugabe.

Ameeleza katika uchaguzi huo wa kihistoria Zimbabwe inatarajia kumwona kiongozi mpya na utakuwa uchaguzi wa kwanza bila kuwepo kwa Robert Mugabe kama mgombea tangu nchi hiyo ilipopata uhuru kutoka kwa Uingereza mwaka 1980.

Aidha Mnangagwa (75) anayeaminika anaweza kuwa Rais ajaye amewahakikishia wanazimbabwe kuwa uchaguzi huo utakua wa amani na wazi na tayari amealika vyama vya siasa nchini humo kwa majadiliano zaidi.Ikumbukwe Robert Mugabe alizaliwa tarehe 21 Februari 1924 huko Salisbury Zimbabwe, ni mwalimu kitaaluma anayeaminika kuwa na Shahada saba kutoka Vyuo Vikuu.

Mugabe aliongoza vita dhidi wakoloni wakati Zimbabwe  ikijulikana kama Rhodesia na alifungwa kwa miaka 10 kutokana na hotuba yake ya 1964 ambayo iliwaghadhabisha wakoloni kwa kuwaita wachochezi na mwaka 1974 aliachiwa huru.Kuhusu uongozi Mugabe alianza 1974 baada ya kuachiwa huru kwa kuwashinikiza Waingereza kusitisha utawala Rhodesia.

 Mwaka 1979 alitorokea Msumbiji na aliporejea nchi hiyo ilipata uhuru mwaka 1980 na Mugabe alikuwa Waziri Mkuu kupitia ZANU PF.Mwaka 1987 Mugabe alichukua kiti cha urais na kuhudumu kwa miaka 37 hadi Novemba mwaka 2018 ambapo jeshi la nchi lilipompindua na makamu wake kukaimu nafasi hiyo.

Na hiyo ni baada ya Rais Mugabe kumfuta makamu huyo kazi kwa kuamini utawala wa Mnangagwa ni haramu na fedheha kwa nchi yao

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...