Na Zainab Nyamka, Globu ya jamii
SHIRIKISHO la Mpira Kikapu Tanzania(TBF) imetangaza rasmi tarehe
ya mashindano ya kikapu ya FIBA Zone V U18 (Wanawake na
Wanaume ) kuwa yanatarajiwa kuanza June 17 hadi 22 2018 hapa
Jijini Dar Es Salaam, Tanzania.
Rais wa TBF Pharess Magesa amesema matarajio yao ni kuwa
mmoja kati viongozi wetu wakuu wa nchi ndyie atakuwa mgeni
rasmi wa mashindano hayo na yatarushwa mubashara (live) siku
zote za mashindano na vituo vyote vikubwa vya TV na Radio
ambavyo wametuma maombi.
Magesa amesema gharama za maandalizi ya timu zetu mbili za
Taifa na gharama za kuandaa mashindano haya ni kubwa, na tayari
kuna wadau wameshajitokeza kutoa ahadi na wengine
wameshasaidia.
"Hadi sasa hivi TBF ina upungufu wa takribani Sh.milioni 100, kati ya
hizo Sh.milioni 60 ni za kuandaa mashindano na Sh.milioni 40 ni za
kuweka timu zetu 2 za wanawake na wanaume kambini na kununua
vifaa vya michezo zikiwemo Jersey za kucheza na za mazoezi, truck
suits, viatu, socks, mipira na madawa,"amesema Magesa.
"Pia, tuna mahitaji mengi ili kufanikisha matengenezo ya uwanja wa
ndani wa Taifa (indoor) ukiacha kuvuja paa na kukatika kwa umeme
ambako kutadhibitiwa na msaada ulitolewa na Mkuu wa Mkoa wa
Dar es Salaam Paul Makonda,"amesema.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...