Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi amekutana na Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Dkt. Reginald Mengi ili kuzungumza na kutambua fursa zinazopatikana za uwekezaji katika sekta ya Ardhi nchini.
Dkt. Mengi amekutana na Mhe. Lukuvi ofisi kwake kanda ya Dar es salaam ambapo wamejadili mambo mbalimbali ambayo Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imeyafanya katika sekta ya ardhi ambayo na kutoa fursa kwa wawekezaji wa ndani kuwekeza kwa urahisi.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi (kushoto) akizungumza na Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Dkt. Reginald Mengi(kulia) alipomtembelea ofisini kwake kanda ya Dar es salaam .
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akipokea nyaraka ya makusudio ya kuwekeza katika ardhi kutoka kwa Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Dkt. Reginald Mengi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...