Na Bashir Nkoromo, Geita.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania Dk. Edmund Mndolwa ameahidi kuupatia ufumbuzi mgogoro wa machimbo ya dhahabu wa Lwamgasa mkoani Geita uliopo kati ya Jumuuya ya Wazazi mkoa wa Geita na Jumuiya ya Wazazi mkoa wa Mwanza.

Mgogoro huo umeibuka tangu Geita ilipomegwa kuwa mkoa, na hivyo leseni ya machimbo hayo yaliyopo Geita huhodhiwa na Jumuiya Wazazi Mwanza huku machimbo yenyewe yakiwa kwenye mkoa wa Geita.

Mvutano wa umiliki wa machimbo hayo umekuja kutokana na Jumuuya ya Wazazi Geita kuona kuwa ni rasilimali yake lakini haipati chochote badala yake wanaofaidika nayo ni Mwanza. "Ninayo majembe (viongozi) ambao nikikaa nao tutaumaliza mgogoro huu, na hii ni Geita isiwasumbue sana hasa mkizingatia kuwa mali za jumuia ni mali za Chama". alisema Dk. Mndolwa.

Dk. Mndolwa ambaye alikuwa akizungumza katika kikao cha ndani na Wajumbe wa Halmashauri kuu ya CCM mkoa wa Geita na Wajumbe wa Mabaraza ya Jumuiya za Chama kutoka wilaya za mkoa huo alisema, moja ya tatizo ni kwamba rasilimali nyingi za Chama na jumuiya zake kwa sasa nyingi zimo mikononi mwa watu binafsi.

Alisema kwa kuwa CCM imelitafutia ufumbuzi tatizo hilo sasa litakwisha na mali zote zitanilikiwa na Chama kikamilifu na hivyo migogoro mingi kuhusu mali za Chama itapungua au kuisha kabisa .Dk. Mndolwa alisema yeye pamoja na safu ya uongozi wake watahakikisha Jumuiya ya Wazazi inakuwa Jumuiya ya mfano zaidi Kwa kuhakikisha rasilimali zake zinakuwa endelevu na hivyo mambo mengi ndani ya Jumuiya hiyo yatakwenda vizuri.

" Jumuiya hii kama ni kipele sasa kimepata mkunaji, nataka niwahakikishie wana CCM wenzangu kwamba sikuja katika Jumuiya hii kuganga njaa, nimekuja kufanya Kazi bila kubabaisha, ninyi wenyewe ni mashahidi tangu uongozi huu mpya mishahara inawahi na mambo mengi ikiwemo bima ya afya Kwa watumishi wetu tumehakikisha tunasimamia vilivyo" Aliseama

Dk. Mndolwa alisema Tanzania chini ya Rais Dk Magufuli had I kufikia 2023 itakuwa imeingia katika hadhi ya uchumi wa kati

Dk Mndolwa yupo katika ziara ya mikoa ya Kagera, Geita, Mara, Simiyu na Singida kushukuru Kwa kuchaguliwa na pia kuwatambulisha Makamu wake upande wa Zanzibar Haidar Haji Abdallah na Katibu Mkuu mpya wa Jumuiya ya Wazazi Erasto Sima ambao ameambatana nao kwenye ziara hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...