Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Mhandisi Isack Aloyce Kamwelwe
(MB), ametembelea na kuona miradi mbalimbali inayotekelezwa Mkoani
Geita akiambatana na Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe. Mhandisi Robert Gabriel,
Mkuu wa Wilaya ya Chato Mhe. Shaaban Ntarambe, Mkurugenzi wa Mamlaka ya
Bandari Mhandisi Deusdedith Kakoko, pamoja na Meneja wa TANROADS Mkoa
wa Geita Mhandisi Harun Senkuku.
Miradi
aliyoitembelea ni pamoja na Bandari ya Nyamirembe iliyoko kijiji na
Kata ya Nyamirembe Wilayani Chato ambayo ilikua ikitumika tangu enzi ya
Mkoloni ambayo kwa sasa haifanyi kazi. Waziri amewaeleza wananchi
wajiandae kufurahi kwani muda si mrefu bandari hiyo itafufuliwa na
kuanza kazi; ni baada ya kujitokeza kumlaki kwa fuaraha baada ya kumuona
akitembea kwenye bandari hiyo.
Amesema
“mwezi wa nane mwaka huu tunasaini mkataba, tunairudisha Bandari ya
Nyamirembe. Na sasa tunajenga meli kubwa, itakayokuwa na uwezo wa kubeba
abiria elfu moja mia mbili (1,200), mizigo tani mia nne (400) ambayo
itapita hapa kwenda Bukoba ndiyo maana kituo hiki lazima tukijenge na
mkandarasi anaingia hapa mwezi wa nane.
Hivyo ni ushindwe mwenyewe
mwananchi kwa sababu sasa meli itakuwepo, barabara ya lami ipo, kiwanja
cha ndege kinaendelea kujengwa unataka nini tena?” alimaliza kwa
kushangiliwa na wananchi.
Kisha, Waziri ametembelea na kujionea maendeleo ya hatua ya ujenzi wa
barabara ya Bwanga – Biharamulo yenye urefu wa kilomita sitini na saba
(Km.67) inayojengwa kwa kiwango cha lami na kufurahishwa na hatua
iliyofikiwa baada ya kupewa taarifa kuwa, barabara hiyo imeshajengwa
hadi kilomita hamsini na saba (Km.57) hivyo bado kilometa kumi (Km.10)
ili iweze kukamilika.
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...